Mjue Mtakatifu Peter wa Verona shahidi

Mjue Mtakatifu Peter wa Verona shahidi

Alipingana na mafundisho ya uwongo toka utoto wake

MTAKATIFU Peter alizaliwa Verona mwaka 1205. Wazazi wake walikuwa watu wenye kupinga mafundisho ya Kanisa Katoliki. Hata hivyo wazazi wake walimpeleka katika shule ya Katoiliki kwa sababu kulikuwa hakuna shule nyingine katika jiji hilo isipokuwa shule ya katoliki.
Mara alijifunza si kwa kusoma na kuandika pia hata nasadiki. Toka utoto wake alipinga mafundisho ya uwongo
Siku moja, wakati anakaribia miaka saba  alipokuwa anakuja toka shuleni alikutana na mjomba wake aliyekuwa mpinga mafundisho ya Kanisa Katoliki alimuuliza nini alichojifunza. Mvulana  huyu alimjibu,  nimejifunza kanuni ya imani “nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia”.
Hivyo ndivyo alivyomjibu mjomba wake, na mjomba wake akamwambia hii si sawa  na alimsisitiza aache kuamini kuhusu hili. Lakini Peter alikataa kupotoshwa na maneno ya kudhihaki ya kudharau vitu vitakatifu. Mjomba wake baada ya kugundua kuwa mwanae huyu anapingana na mafundisho ya uwongo aliamua kutompeleka tena kusoma katika shule ya kikatoliki.
Hata hivyo baba yake aliamua kumpeleka Bologna kuendelea na masomo. Pale alikuwa na nafasi ya kusoma vitabu vya kikatoliki ambavyo vilimsaidia kuongeza ufahamu wake na kumuimarisha katika imani yake. Katika mji huu alifahamiana na mtakatifu Dominiki mwazilishi wa wadominikani, na alimuomba ili aweze kumuingiza katika jumuiya yake mpya aliyoanzisha.
Ombi lake lilikubaliwa na aliguswa na maisha ya ndani ya kiroho, kwa kipindi kifupi alikuwa mfano wa kila fadhila. Baada ya kumaliza masomo na kupadirishwa, alichaguliwa kuhubiri na  aliichukulia kazi hii kwa  mafanikio mazuri na alijulikana katika Italia yote kwa jina la mtume.
Siku moja alipokuwa katika katika sala, alikuwa amezama ndani zaidi katika sala, mara mabikira watatu na mashahidi walimtokea, walikuwa Mtakatifu Agnes, Catherine, Cecilia, waliongea naye kama binadamu mwingine anavyozungumza na wenzake, mtawa mmoja bila kufikiria  alipita alisikia walichoongea na kwenda kutoa taarifa kwa Baba mkuu wa nyumba kwamba Peter amewaingiza wanawake katika chumba chake. 
Baba mkuu bila hata kudadisi alichukulia taarifa hii kama kashfa ndogo, alimuita Peter mbele ya wenzake na kumwambia kuhusu kitendo hicho kama kashfa. Peter alikuwa mnyenyekevu kueleza au kuzifunulia neema ambazo alizopata toka mbinguni, huku  akipiga magoti, na “kusema mimi ni mwenye dhambi na Nipo tayari kupokea adhabu”.
Haya maneno yalichukuliwa kama kama ni ukweli aliokubali toka kwa mashataka aliyopata toka kwa ndugu zake na alipewa adhabu kwenda kwenye Konventi nyingine na kuwekwa kama mfungwa na kutopewa nafasi ya kuhubiri au kukutana na mtu yeyote. Pamoja na kutokewa na kuongea na watakatifu hao, na pia kwa kushtumiwa na ndugu wenzake yeye alikubali adhabu hiyo kwa unyenyekevu na hata hajalalamika lakini kwa uvumilivu alikuwa na tumaini kwamba ipo siku kwa muda wake Mungu atamfunulia.
Siku moja alijilaza kifudifudi na kulia mbele ya msalaba na kusema,  “O, Mungu wangu kwanini kitu hakijulikani bado kwa mtu asiye na hatia? Baada ya hapo alisikia sauti ikimwambia, jifunze toka kwangu kwa unyenyekevu kuvumilia msalaba uzito ambao huwezi kuulinganisha na wangu”. 
Baada ya kusikia maneno hayo alijazwa na furaha na kuamini kwamba hana kitu chochote zaidi bali kuteseka kwa ajili ya Kristo.
Kwa muda mrefu Mungu alimletea mwanga mtu wake asiye na hatia kwa ndugu zake ambao walimshutumu na hatimaye alipokelewa na kuanza upya kazi yake ya mwanzo na kuendelea kuhubiri kwenye sehemu mbalimbali za mji na vijijini Mpaka kifo chake. Aliwabadilisha wenye dhambi wengi na  wengi wale waliokuwa wanapinga mafundisho ya kanisa  na kuhufahamu ukweli.
Wakati wa miaka mingi ya kufanya kazi yake ya kuhubiri, Mungu alimfunulia  kwamba kifo chake kipo karibu na kitakuwa kama alivyotamani. Siku moja watu waliokuwa wawili ambao walikuwa wameazimwa na watu wasioamini mafundisho ya kanisa walimtegea sehemu ambayo alikuwa anapita ili wamdhuru kwenye kichaka.
Walimpiga kichwani na upanga mara nyingi. Chini ya ardhi alichovya kidole chake kwenye damu zilizokuwa zinamtoka na kuandika kwenye udongo. “Nasadiki kwa Mungu Baba” na kuinua macho yake juu na kusema “mikononi mwako bwana naiweka Roho yangu”. Na kufariki. Wale wauaji waliondoka huku walimchoma katika moyo wake. 
Mwili wake ulizikwa katika kanisa la Mt.Eustorgius. Miujiza mingi ilifanyika na ilimpelekea Papa Innocent IV kumtangaza mtakatifu.

Imetayarishw na padre. Theophil. C.Wabukundi, OCD. Wa Shirika la Karmeli, Paroko Msaidi Parokia ya Mt. Theresia wa mtoto Yesu Mbezi Mwisho, na Mkurugenzi wa Miito. 0764038597, theoocd@gmail.com

Comments

  1. I wishes to joined in your carmelite congregation father

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU