••TANZIA••

Kwa masikitiko na huzuni kubwa, tunawataarifu kifo cha Padre FABIAN NDERUMAKI, padre wa jimbo katoliki la Moshi.

Padre Fabian Nderumaki alifariki dunia tarehe 02/04/2016 saa nne usiku.
Padre Nderumaki hadi mauti yanamfika alikuwa ni Paroko wa Parokia ya Himo jimboni Moshi.

Kabla ya kuteuliwa na baba askofu kuwa paroko wa Himo, Padre Fabian Nderumaki alikuwa Gombera(Rector) wa seminari ndogo ya Mtakatifu Yakobo-Kilema(St.James Seminary)

Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliofanya naye kazi seminari ya St.James na waamini wote ambao Padre Fabian Nderumaki amewahi kuwahudumia katika parokia zao kama padre enzi za uhai wake. Pia kwa mapadre, watawa na wote waliowahi kufanya nae kazi

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe milele na milele, AMINA.


ROHO YA MAREHEMU PADRE FABIAN NDERUMAKI IPATE REHEMA KWA MUNGU, APUMZIKE KWA AMANI.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU