UZINDUZI WA MIAKA 20 YA REDIO MARIA WAFANA DAR ES SALAAM..






















Matukio mbalimbali ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania tangu kuanzishwa kwake. Uzinduzi huo umefanyika katika Kanisa la Mt. Maxmilian Maria Kolbe Parokia ya Mwenge Jimbo Kuu Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na waamini kutoka ndani na nje ya Parokia ya Mwenge wakiwemo waanzilishi wa Redio hiyo hapa nchini, Marafiki pamoja na wadau mbalimbali.

Adhimisho la Misa Takatifu liliongozwa na Askofu wa Jimbo Mtwara Mhashamu Titus Mdoe akishirikiana na Paroko wa Parokia ya Mwenge na Msaidizi wake Padri Sixbert Heri, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza Padri Cathibert Sasagu Maganga na Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padri John Maendeleo.

Radio Maria ilianza kurusha matangazo yake nchini mwaka 1996 ambapo makao makuu yalikuwa Jimbo Kuu Songea na sasa makao makuu yapo Mikocheni Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Kilele cha maadhimisho haya kinatarajiwa kuwa Julai 31 mwaka huu.

Adeline,TEC


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU