Zaidi ya watu 110 wameungua moto na wengine 350 kujeruhiwa



Baba Mtakatifu Fransisko amepokea kwa masikitiko makubwa habari za ajali ya moto uliotokea Jumamosi tarehe 9 Aprili 2016 kwenye Hekalu la Puttingal, eneo la Paravoor huko Kerala nchini India na kusababisha zaidi ya watu 110 kupoteza maisha na wengine 350 kupata majeraha makubwa. Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, anapenda kutuma salamu zake za rambi rambi kwa wote waliokumbwa na msiba huu mzito.

Baba Mtakatifu anawaombea majeruhi waweze kupona haraka na hivyo kurejea katika maisha yao ya kawaida na marehemu waweze kupata faraja na huruma ya Mungu mbinguni. Mwishoni, Baba Mtakatifu anaiombea India baraka, nguvu na amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU