BALOZI WA BABA MTAKATIFU NCHINI ASKOFU MKUU FRANSISKO PADILLA AKITABARUKU KANISA JIPYA JIMBO KATOLIKI KAHAMA


Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akiweka jiwe la msingi katika jengo la masomo ya TEHAMA katika shule ya wasichana ya Mtakatifu Theresia wa Avilla Jimbo Katoliki Kahama katika ziara yake ya kichungaji ya siku tano jimboni humo (Picha na Patrick Mabula)

Kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima 

Watoto wa shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu wa Yesu wakiongoza maandamano siku ya kutabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima  jimbo la Kahama  (Picha na Patrick Mabula)



Padri Andrew Maziku akiwa amebeba masalia ya Watakatifu  ya kuzikwa kwenye  Altare wakati wa maandamano ya kuelekea kanisa jipya la Ekaristi Takatifu -Kabuhima jimbo la Kahama  wakati wa misa ya kutabaruku kanisa hilo (Picha na Patrick Mabula)




Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akikata utepe kufungua kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima Jimbo Katoliki Kahama  lenye uwezo wa kuingiza waamini zaidi ya 1,500  kwa  mara moja  (Picha na Patrick Mabula)



Paroko wa Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima  Padri Salvatore Guerrera  akifungua rasmi mlango wa kanisa jipya  baada ya kupewa ufungua  na Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini  Askofu Mkuu Fransisko Padilla baada ya kukata utepe (Picha na Patrick Mabula)

Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla  akizika masalia ya Watakatifu katika Altare ya Kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima  jimbo la Kahama alipolibariki na kulitabaruku. Katikati ni Askofu wa Jimbo la Kahama Mhashamu Ludovick Minde na kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo Padri Salvatore Guerrera  (Picha na Patrick Mabula)




Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akipaka mafuta matakatifu ya Krisma katika Altare alipokuwa akitabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima, kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo Padri Salvatore Guerrera (Picha na Patrick Mabula)

Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akiweka ubani kwenye karai yenye mkaaa juu ya altare  alipokuwa akitabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima Jimbo Katoliki Kahama.  Pembeni yake ni Askofu Ludovick Minde wa jimbo la Kahama (Picha na Patrick Mabula)

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU