Mtakatifu Gemma Galgani


Alipata neema ya kupata Madonda Matakatifu

Mtakatifu Gemma Galgani
GEMMA Galgani alizaliwa Machi 12, 1878 kwenye kijiji kidogo cha Tuskan karibu na Lucca, alikuwa mmoja kati ya watu ambao Mungu mara kwa mara alimchagua kuwa shahidi maalumu wa Mateso ya Yesu , ambapo aliweza kuyapata.
Baba yake alikuwa mkemia na mtu mzuri sana, mama yake pia alikuwa mwanamke mtakatifu. Familia yao walikuwa nane ambapo Gemma yeye  alikuwa mtoto wanne, akiwa na umri wa miaka saba Gemma alifiwa na mama yake mzazi.
 Ilikuwa katika mafundisho ya mwanzo kabisa Gemma aliweza kuwa na uchaji wa mateso ya bwana.  Katika umri wa miaka tisa alipata Komunio ya Kwanza, alishindwa kueleza namna gani alivyoshindwa kujieleza kipindi hicho alichounganika kati ya roho yake na Bwana.
Gemma alipenda  ukimya na upweke na alikuwa mara nyingi sio muongeaji. Usichana wake ulitawaliwa na kuteseka kwa mambo mbalimbali kama vile majaribu ya ndani, vilevile ugonjwa ambapo ulisababisha hata daktari kumkataza kurudi tena shuleni mwaka 1894, pia hali mbaya ya kiuchumi ya ndugu zake, madharau ya watu waliomcheka kutokana na mazoea yake ya kidini.
Gemma alitamani sana kuwa mtawa, lakini alikataliwa mara mbili na Wakuu wa Mashirika mawili tofauti ya kitawa kwa kigezo cha afya yake mbaya. Pamoja na hayo aliweza kuishi maisha ya sala na kiroho sana kama mkristo mlei. Siku moja baada ya kukomunika, Bwana Yesu alimtokea na kusema naye; “Gemma ninakutarajia kalvari.” Mawazo, maneno na matendo yake yalimwelekea Yesu tu. “Alimwambia Bwana utakapotaka kunitesa, tusifanye kelele, bali mambo yote yawe siri. Mimi nataka kukupenda kwa msalaba wako. Sitaki kitu kingine ila kimoja tu :  nataka kukupenda”.
Baada ya maumivu ya ugonjwa muda mrefu aliweka nadhiri ya usafi wa moyo na ilipokuwa februari 1899 alijiunga na Novena ya Mtakatifu Margareth Mary.
Mtakatifu Gabrieli alimtokea na kumuahidi kufanya novena pamoja naye. Walifanya novena hiyo kila siku usiku, akisali pamoja naye. Aliipeleka kwa baba yake wa kiroho, alipokea komunyo na Rose akiwa kitandani na hatimaye kupona kabisa.
Muda mfupi baada ya kupona ugonjwa wake, alitaka kuwa mtawa katika Shirika la Passonist lakini afya yake haikumruhusu.
Siku ya mkesha wa sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mwaka 1899, akisaidiwa na malaika wake mlinzi na  Mama yetu Bikira Maria, Gemma alipata toka kwa Bwana Madonda Matakatifu na yalikuwa yanamtokea kila Alhamisi jioni hadi siku ya ijumaa mchana.
Mapadri wa passionisti walimsaidia kama washauri wake wa kiroho. Yalitokea mara kwa mara miaka 1899 na 1901 yalikuwa yakichuruzika damu nyingi sana na kumsababishia maumivu makali mno, hata gemma alikuwa akidhani atazimia roho.
Alipata maono, ufunuo, na maunganiko yalikuwa mara kwa mara, na alizungumza mara kwa mara na Malaika wake mlinzi aliyemuona na pia aliweza kuwa na zawadi ya unabii na ufahamu usio wa kawaida sifa za utakatifu wake zilienea nje na  fadhila nyingi zilipatikana kupitia sala zake.
Alifariki Aprili 11 1903 akiwa na miaka ishirini na tano, alipojitoa mwenyewe kama sadaka kwa wenye dhambi hasa kwa mapadri wenye mapungufu. Kabla ya kufikia miaka arobaini alitangazwa Mtakatifu na Papa Pio XII siku ya sikukuu ya kupaa kwa Bwana 2 Mei mwaka 1940.

Imetayarishwa na Padri wa shirika la Karmeli, Paroko Msaidizi Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Mbezi Mwisho na Mkurugenzi wa Miito. Kwa msaada wa vitibu vya, Saint Companions for Each Day, Oxford Dictionary of saints, Maisha ya watakatifu. 0764038597, theoocd@gmail.com

Comments

  1. Hakika historia ya Mtakatifu Gemma imenigusa sana na kunipa faraja kuu sababu mama yangu anaitwa Gemma na alikuwa mtu wa sala pia alipata mateso ya kuumwa kupararazi hata kushindwa kutembea kwa miaka 5 baada tu ya baba yangu kufariki. Na katika kuumwa kwake aliishikiria imani na hata ugonjwa wake ulituimarisha kama familia na hata kifo chase Mungu mwema aliweza nionyesha na kunipa nguvu na mguso mkubwa wa kumshukuru MUNGU kuliko lawama na hata baada ya kifo chake MUNGU mwema alituangazia nuru ya yale yaliyokuwa yanatupa huzuni. Sasa hii inanipa nguvu ya kuona jina la Gemma lina nguvu katika kristo na mama ameungana na Gemma akiwa nae ni mtakatifu na muombezi wetu.

    ReplyDelete
  2. hakika ni historia nzuri sanna na inafundisha

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU