KIPAIMARA:SERENGETI WAIMARISHWA




ASKOFU wa Jimbo katoliki Musoma Michael Msonganzila ametoa sakramenti ya kipaimara kwa waamini wa Parokia ya Serengeti inayoongozwa na Padri Bernald Chegere,iliyopo ndani ya hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Serengeti,ikiwa ni sehemu ya kuwasogezea huduma ya kiroho wafanyakazi waliomo ndani ya hifadhi hiyo ambao ni vigumu kuifuata huduma hiyo mjini Mugumu.

Pia Askofu Msonganzila ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la kanisa lililopo parokia ya Serengeti iliyopo ndani ya hifadhi hiyo ili kuifikisha haraka huduma ya kiroho kwa watumishi wa idara mbalimbali waliomo ndani ya hifadhi.

Victoria Modest,Musoma

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU