Waraka mwingine wa Papa Fransisko kutolewa Aprili 8


Waraka mwingine wa Baba Mtakatifu Fransisko juu ya Sinodi ya Familia unatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa Aprili 8, huku waraka huo ukipewa jina la  “Amoris Laetitia”, yaani “Furaha ya upendo”
Waraka huo utatolewa rasmi na Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Kardinali Lorenzo Baldisseri, na Askofu Mkuu wa Vienna Kardinali Christoph Schönborn.
Miongoni mwa watu watakaohudhuria tukio hilo ni pamoja na wanandoa Prof. Francesco Miano, ambaye ni Mhadhiri wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Roma (Tor Vergata), na Prof. Giuseppina De Simone.
Itakumbukwa kuwa hapo mwaka jana Katibu Mkuu wa Vatikani Kardinali Pietro Parolin alisema kuwa Waraka huu wa Papa utakuwa unajikita katika kuhitimisha Sinodi, kama ilivyo utamaduni wake.

Sinodi juu ya familia iliyofanyika kwa takribani wiki 3 iliwakutanisha Maaskofu 270 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu utume wa familia na changamoto zake.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU