MSIBA MZITO: TEC yaomboleza
BAraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC limepata pigo baada ya kuondokewa na Mkuu wa Idara ya Uchungaji Padri Galus Marandu wa Shirika la Roho Mtakatifu(C.SS.P) aliyefariki dunia Jumapili tarehe 26 Machi 2017 Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Katika Ibada ya Misa Takatifu ya kumuaga Padri Marandu iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili TEC, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema Kanisa Katoliki nchini limepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mtendaji mahiri na mwajibikaji mwenye ubunifu katika kuhudumia jamii. “Katika uhai wake, Padri Marandu alikuwa mchapa kazi na alifanya kazi kwa umakini na ufanisi mkubwa. Kipindi cha miaka 15 aliyofanya kazi TEC, Padri Marandu ameacha matunda yanayoonekana wazi na jamii inajivunia hasa kwa kuhakikisha anawajenga watu katika upendo, amani, umoja na mshikamano kwa kuwaunganisha watu wa Dini mbalimbali kuwa kitu kimoja kwani jambo hilo si la mchezo na k...