WAKRISTO NA WAISLAMU WALAANI UGAIDI

Kutoka Italia na Ufaransa.Siku ya Jumapili nchini Italia Waislamu na Wakristu wameweza kujumuika kwa pamoja na Kusali katika parokia mbali mbali za Makanisa Katoliki.
Wamefanya hivi ili kupinga mauaji yaliyofanywa ndani ya kanisa la Mtakatifu Etienne-du-Rouvray nchini Ufaransa. Pia wamefanya hivi ili kudumisha amani na kupinga ugaidi unaoendelea kufanywa kila kukicha katika nchi mbali mbali ulimwenguni na kuuwa watu wasio na hatia.
Misa hii imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maria lililopo Roma ambapo watu elfu 15 waliweza kuhudhuria misa hiyo wakiwemo maimamu mbalimbali pamoja na Rais wa Jumuiya ya Dunia ya kiarabu nchini Italy Foad Aodi.

 Michael Minja










Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI