PAPA FRANSISKO KUZURU ENEO LILILOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARDHI
Papa Fransisko anatarajia kuzuru maeneo yalioathiriwa na tetemeko la ardhi huko nchini Italia hivi karibuni na kuwafariji wahanga.
Katika sala za kila jumapili St. Peter’s Square, Papa amesema anatarajia kuwa karibu kiroho na wahanga wa tetemeko la ardhi hasa maeneo ya Latium, Marches na Umbria.
Amesema kanisa lipo nao katika kipindi hiki kigumu cha mateso na hofu.
Idadi ya vifo vilivyosababishwa na tetemeko la ardhi juma lililopita imefikia 300.
Papa amepongeza jitihada zilizofanywa na wote waliotoa misaada mbalimbali akisema mshikamano mkubwa una faida katika kuondokana na majaribu yanayoumiza.
Comments
Post a Comment