PAPA FRANSISKO ATOA RAI


Baba Mtaktifu Francisko ametoa mwaliko kwa watu wote kwamba, katika mwaka huu wa Jubilei ya Huruma , ni jambo jema kupita katika Mlango Mtakatifu , Mlango wa Huruma ya Mungu , kama ilivyotokea katika mlango wa kijiji cha Nain. Papa alitoa mwaliko huo wakati akitoa katekesi yake kwa mahujaji na wageni walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, mapema Jumatano hii.Katika Katekesi hii amefafanua juu ya muujiza wa Yesu ambamo alimwonea huruma mwanamke mjane aliyekuwa amefiwa na mtoto wake" Injili ya Luka 7: 11-17.  
Akizitafakari aya hizo alisema , kwa hakika muujiza huu wa Yesu kumfufua kijana mdogo si tu unatuonyesha uwezo wa Yesu katika kufanya miujiza lakini hasa inaonyesha huruma ya Yesu kwa mama wa kijana huyo. Huruma ya Yesu kwa mjane huyo aliyekuwa amempoteza mme wake na sasa anakwenda kumzika mtoto wake . Ni wazi mama huyo alikuwa amezongwa na huzuni kubwa, ilikuwa ni kilio kikubwa kwa mjane huyo,  na Yesu anamwonea huruma na kumfufua mtoto huyo. 
Papa aliendelea kutoa mafundisho juu ya muujiza huu , ambamo Mwinjilisti Luka kwa namna ya kipekee ameelezea mengi juu ya safari hii ya Yesu katika Kijiji cha Nain, kwamba Yesu wakati akiingia katika mlango wa kijiji , akiwa na wanafunzi wake , alikutana na watu waliokuwa wamebeba jenaza la mtoto akiwepo pia mama wa marehemu aliyekuwa akilia kwa nguvu, mwanamke mjane. Yesu alivyomwona mjane huyo akilia kwa huzuni kubwa,  alishikwa na huruma na kumfariji akimwambia " mama usilie". Yesu alilikaribia jeneza na kuligusa na wachukuzi wa jeneza walisimama tuli. Yesu akiongozwa na huruma, aliyaona mateso ya mjane na hivyo akaona haja ya kumfufua mtoto huyo. Papa amesema, hapa tunaona kuwa Yesu anakabiliana na kifo uso kwa uso, kama alivyofanya wakati wa kifo chake msalabani.Yesu hakukihofia kifo, lakini anakiitisha na kumfufua mtoto.
Baada ya maelezo hayo Papa aliendelea kuainisha uwepo wa tukio hili katika lango la Kijiji cha Nain na maadhimisho ya mwaka wa Huruma ambamo Waamini wanatakiwa kupita katika Mlango Mtakatifu.Amesema kuwa katika wakati huu wa maadhimisho ya waka wa Jubilee ya huruma, ni vyema kwa kila mmoja kwenda kupita katika Mlango Mtaktifu , Mlango wa Huruma , na kukutana na Yesu kama ilivyokuwa katika mlango wa kijiji cha Nain, ambako Yesu alikutana na mwanamke mjane aliyekuwa akitokwa na machozi na kumwonea huruma, na kuichukua huzuni ya mama huyo ktiak moyo wake.  Na ndivyo ilivyo pia kwetu kaiak wakati huu , twende kupita katika Mlango Mtakatifu tukiwa tumebeba hali zote za maisha, furaha, huzuni, mateso , mafanikio, kushindwa , mashaka na hofu, vyote ni kuviweka mbele ya  huruma ya Bwana.
Papa alieleza na kuonyesha imani yake kwamba, kwa hakika katika Mlango Mtakatifu kuna kukutana na Bwana . Bwana anataka kukutana na kila mmoja wetu , ili kumpa neno la faraja kama ilivyokuwa kwa mwnamke mjane , kutuambia "usilie". Ameutaja Mlango Mtakatifu kuwa ni mahali pa makutano kati ya maumivu ya kibinadamu na huruma ya Mungu.Ni mahali ambapo makutano kati ya  maumivu ya kibinadamu na huruma ya Mungu huvunja kizingiti kinachoifanya roho isinzie . Ni mahali pa kuisikia kweli huruma ya Mungu, kuna sauti ya huruma inayotuita kutoka katika wafu kama ilivyokuwa kwa kijana aliyekuwa amefariki( mustari 14)  .. Katika Mlango Mtakatifu kila mmoja wetu anaambiwa na Yesu"amka" . Mungu anatutaka tusimama katika miguu yetu na tuwe imara. Papa aliongeza kwamba Mungu alituumba na kututaka daima tusimame imara , ndiyo maana Yesu anatuonyesha huruma yake kwa ishara ya uponyaji , anataka kutuponya dhidi ya mateso yetu. Pamoja na kwamba tuna udhaifu wa kuanguka mara kwa mara katika dhambi, yeye hachoki kutuinua kwa mkono wake wa huruma. 
Papa alieleza na kusisitiza kwamba, ni muhimu kuiskiliza sauti ya Bwana inayotutaka kuamka. Na hivyo neno hili amka linakuwa na umuhimu wa kipekee katika maisha yetu. Ni neno lenye kutupa faraja na matumaini , na huifufua mioyo iliyochoka , kuweza kufungua mtazamo mpya katika maisha ya duniani, maisha ya dhiki , mateso na kifo. Papa alieleza na kuhimzi sote twende kupita katika Mlango Mtakatifu ambako kuna hazina isiyokuwa na kikomo ya huruma ya Mungu . Yesu kwa huruma anatuumbia moyo mpya , moyo ulioponywa kwa matendo yake ya huruma . Kinachohitaji si sisi kuianza safari ya kuelekea katika Mlango Mtakatifu, kwenda kukutana na huruma ya Yesu na kuionyesha huruma hiyo kwa wengine , na hasa wenzetu waliozongwa na dhiki na huzuni kubwa kama ilivyokuwa kwa mwanamke mjane. Papa Francisko alisisitiza.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI