TETEMEKO LA ARDHI ITALIA:PAPA FRANSISI AWAOMBEA WAHANGA

Baba Mtakatifu Francisko  akiwa amehuzunishwa na vifo,  mahangaiko na maombolezo ya watu walioathirika na tetemeko la aridhi lililotokea katika mkoa wa Marche, Umbria na Lazio hapa Italia , usiku wa kuamkia Jumatano hii, aliamua kuahirisha katekesi yake kwa mahujaji na wageni na badala yake aliongoza Ibada ya Rosari katika uwanja wa Kanisa Kuu la Makatifu Petro, kwa nia ya kuwaombea  waliopoteza maisha katika tetemeko hili na pia kwa wote walioathitìrika vibaya ambao wamepoteza makazi na mali.

Akitoa maelezo yake kwa watu waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa nia ya kusikiliza katekesi ya Papa, aliwaomba radhi akisema , pamoja na kwamba alikuwa ameandaa katekesi yake kama ilivyo kawaida kwa kila siku ya Jumatano  katika mwaka huu wa Huruma , ambamo anaendelea kuzungumzia ukaribu wa Yesu kwa watu wake ,lakini baada ya kupata  habari  za kutokea tetemeko baya la aridhi lililogonga katikati ya Italia na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha , wengine wengi kujeruhiwa, maafa haya yamepiga moyo wake , na hivyo anapenda kuutumia wakati huu wa katekesi kuonyesha huzuni na mshikamano na karibu wake kwa watu wote waliopatwa na maafa haya ya kushtukiza.  Na hasa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao  na wale ambao bado wana mshituko mkubwa na hofu kubwa.
Baba Mtakatifu ameeleza akirejea taarifa kutoka kwa Meya wa eneo la Amatrice, akieleza kwamba sehemu hiyo imeharibiwa vibaya na kati ya waliofariki wamo pia watoto , taarifa iliyogusa moyo a Papa .  Hivyo katika hali hii ya majonzi , Papa alipenda kuwahakikisha watu wote wa Accumoli, Amatrice na mahali pengine katika jimbo la Rieti, na Ascoli Piceno na sehemu nyingine za mkoa wa  Lazio na Umbria , kwamba yu pamoja nao katika sala na maombi yake. Na kwamba kutokea katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kanisa linawakumbatia wote kwa upendo wake wa  kimama,  katika wakati huu wa majonzi na mahangaiko.
Aidha Baba Mtakatifu Francisko aliitumia nafasi hii kutoa shukurani zake za dhati kwa  watu wote wa  kujitolea na  kikosi cha ulinzi wa raia, ambao wanafanya kazi kubwa ya kuwaokoa watu kutoka ktiak vifusi vya majengo.  Anaungana nao katiak kazi zao kupitia njia ya maombi m, ili kwamba, Bwana Yesu Kristo,  daima  awe kiongozi wao katika mateso haya ya kibinadamu, na awe mfariji wa wa mioyo iliyohuzunishwa na wapate  amani kwa  njia ya maombezi ya Bikira Maria.
Kwa mujibu wa taarifa za nyakati za mchana kabla hatujaingia studio,  watu 37 wamethibitishwa kufariki katika maeneo mbalimbali ambako tetemeko la aridhi limepiga kwa kishindo cha uzito wa riketi 6.16.1,lakini hasara kamili ya mali zilizopotea bado kujulikana. Ujeruman tayari imetoa  msaada wake wa hali na mali kwa Italia kama alivyotangaza Waziri wa Mamambo ya nchi za nje Frank Walter Steinmeier , akisema katika wakati huu wa majonzi , tunaungana na marafiki zetu wa Italia katika manjozi na  mahangaiko haya.  Na kwamba wako tayari kutoa msaada wote muhimu unaohitajika.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI