"TUWE NA HAMU YA KUPALIZWA MBINGUNI" PAPA
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu hii akiiadhimisha Sikukuu ya Maria kupalizwa mbinguni roho na mwili , alisema inatupa hamu ya kutafakari kwa mara nyingi maisha ya Bikira Maria katika njia yake ya kuelekea Yerusalem ya mbinguni, ambako alikutana na uso kwa uso na Mungu Baba. Papa alitoa maelezo hayo wakati wa sala ya Malaika wa Bwana , mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro hapa Vatican. Katika hotuba yake ya kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, alitafakari Inijili ya Luka 1:39-56 ambayo inaeleza safari ya Maria kwenda kukutana na binamu yake Elizabeth.
Aya hizo, Papa alisema zinatuongoza katika kutafakari kiroho, njia ya maisha ya Maria tangu katika mji wa Yerusalemu na hatimaye kukutana na uso wa Baba na kuuona tena uso wa Mwana wake Yesu. Historia inaonyesha katika maisha yake ya hapa Dunia, maisha ya Maria yalijaa changamoto na uchungu mkali kama ilivyokuwa wakati wa mateso na kifo cha mwanae , katika mlima wa Karvari, aliko shiriki fumbo la ukombozi ulioletwa na mwanae Yesu Kristo. Baada ya kuikamilisha safari hiyo , Mama Maria , anafikia kilele cha mlima wa maisha, ambako alivikwa mwanga wa jua, na mwezi chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Ufunuo wa Yohana 12,1), na hivyo alikivuka vizingiti na kuingia katika nchi ya mbinguni.
Papa alimtaja Mama Maria, kuwa mtu wa kwanza kumwamini Mwana wa Mungu, na ni wa kwanza kuchukuliwa juu mbinguni roho na mwili. Alikuwa ni mtu wa kwanza kumpokea Yesu mikononi mwake kama mtoto binadamu , na pia kuwa wa kwanza kukubaliwa kuingia ndani ya Ufalme wa milele wa Baba . Bikira Maria, msichana mnyenyekevu wa kawaida wa kijijini, anateuliwa na Bwana, kubeba tumboni mwake Neno la Mungu , kwa sababu yeye alikubali kuiishi Injili, na hivyo anaruhusiwa na Mungu, kusimama milele karibu na kiti cha enzi cha Mwana wake. Na hivyo Neno la Mungu linatimia kwamba ”Bwana atawashusha chini wenye nguvu kutoka kAtika viti vyao vya enzi na kuwakweza wanyenyekevu” .
Na hivyo kwa Maria kupalizwa mbinguni linakuwa ni fumbo kubwa katikA mtazamo wa maisha ya kila mmoja wetu kwa siku zijazo. Maria katika ukweli wake , hutufuatilia sisi katika safari yetu ya maisha , tangu wakati wa kupata kubatizwa ambamo tunatoa ahadi ya kufungamana na Yesu katika maisha , kama Mama yake Maria, alivyoandamana na Yesu siku zote.
Papa alieleza na kuomba , katika sikukuu hii ya Mama Maria kupalizwa Mbinguni , na turudie ahadi yetu ya kutembea katika njia inayoelekea katika dunia mpya na mbingu mpya kama mashahidi wa Kristo aliyefufukana kuyashinda mauti , kumshinda nyule mwovu shetani. Kwa hivyo, furaha ya msichana Mnyenyekevu wa Galilaya, inaonekana katika wimbo wake mkuu ,uliomtukuza Mungu, na hivyo unakuwa ni wimbo wa wanadamu wote, wanaotafuta kuonana na Bwana juu mbinguni , wote wanaume na wanawake , viumbe wanaoishi kwa unyenyekevu, ambão wamekaza macho yao juu mbinguni wakitamani pia kupaa pamoja na Mama Bikira Maria na kukutana na Bwana.
Papa alieleza na kuwakumbuka walio katika mateso hasa wanawake waliozidiwa na uzito wa mateso ya kimaisha na vurugu zinazofanywa dhidi yao. Wanawake walioingizwa katika utumwa kwa viburi cha wenye nguvu na mamlaka juu yao , wale wasichana wanaolazimishwa kufanya kazi za kinyama kama ukahaba, wanawake wanalazimika kutoa mwili na roho zao kwa choyo cha watu dhalimu. Aliomba ili kwamba , kwa haraka kwa ajili yao, ipatikane njia inayoweza kuwatoa katika dimbwi hilo la maisha na kupata mwanzo wa maisha mapya ya amani, haki na upendo, wakati wakisubiri mwanzo wa maisha mapya , ambamo wanaweza kukumbatiwa kwa unyenye kevu na upendo wa kweli na huruma nyingi yenye kuwaongoza hadi katika upeo wa maisha ya mbinguni. Papa alisali na kujiweka katika uaminifu wa wa ulinzi wa Bikira Maria , Malkia wa mbinguni, akiomba amani itawale katika njia za njia maisha yetu , hadi hapo tutakapo iona sura ya Mwanae Yesu , katika furaha kamili ya maisha ya mbinguni.
Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alikabidhi kwa mara nyingine tena wasiwasi na huzuni za wakazi katika maeneo mengi ya dunia yanayo athiriwa na uwepo wa migogoro mbalimbali hasa mivutano ya kivita. Alieleza hilo kwa kupeleka mawazo yake kwa wakazi wa eneo la Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ambako hivi karibuni , kulitokea mfumko mpya wa ghasia zilizosababisha mauaji mapya. Aliomba unyenyekevu wa Bikira Maria uguse hisia zote za ufahamu na hamu ya maelewano!
Aidha aliwasalimu kwa upendo mkuu , vijana wote waliotoka Jimbo la Roma na kutoka mataifa mbalimbali , akitaja kwa namna ya kipekee vijana kutoka Villadose, na jumuiya za waamini kutoka Credaro na wale wa Crosara, na kwa mahujaji na wageni waliofika kusali pamoja nae akiwataka Sikukuu njema ya Maria Kupalizwa mbunguni , na pia kwa wote walio katika mapumziko ya wakati wa kiangazi , kwa wagonjwa na waliobaki ktika hali za upweke kutoka na hali zao za kiwmili na kwa wale wote waliyo yatoa sadaka maisha yao katika siku hizi za likizo kwa ajili ya kuwahudumia wahitaji , Papa alitoa salaam zake na kuomba pia wasimsahau katika sala zao kwa kuwa anahitaji maombezi yao.
Comments
Post a Comment