INDONESIA: SHAMBULIZI LA KIGAIDI LASHINDWA KANISANI,PADRI AJERUHIWA
Ingeweza kuwa kama ilivyotokea nchi Ufaransa hivi karibuni, nchini Indonesia katika kanisa la Mtakatifu Joseph mjini Medan, mvamizi mmoja akiwa na kisu ameingia katika misa ya jumapili akijaribu kumdhuru Padri na waamini waliokuwemo kanisani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, hili limekuwa ni shambulio la kigaidi, likilenga kulipua bomu katika mkusanyiko kanisani, lakini hakukuwa na wahanga.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mlipuaji wa bomu alikaa kati ya waamini wakati alipojaribu kulipua bomu la kienyeji, ambalo lililipuka kinyume na makusudio ya mlipuaji. Huku kajeruhiwa, mlipuaji aliweza kumfikia Padri Albert Pandianga(60) na kumjeruhi kwa kisu.
Jeshi la polisi lilifika mapema eneo la tukio na kulidhibiti. Viashiria vya kundi la Islamic State ikiwemo alama yao vimekutwa katika vitu vilivyoachwa na mlipuaji.
Indonesia ni taifa lenye waamini wengi wa dini ya kiislamu kuliko taifa lolote ulimwenguni. Hata hivyo kumekuwepo na baadhi ya makundi yenye msimamo mkali mengine yakiunga mkono ugaidi ambapo mwaka 2002 huko Bali yalitokea mauaji ya halaiki yakihusisha watu 202.
Bernard James
Comments
Post a Comment