PAPA ATETA NA MUASISI WA FACEBOOK



Papa Fransisi amekutana na muasisi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg pamoja na mkewe Priscilla Chan katika mkutano wa faragha uliofanyika kwenye makazi ya Papa huko Casa Santa Marta Vatican.
Waraka uliotolewa na ofisi ya habari ya Vatican umesema Papa na muasisi huyo wamejadili namna ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano kuondoa umaskini, kuhamasisha utamaduni wa makutano, na kusaidia kufikisha ujumbe wa matumaini, hususani kwa watu wasio na usaidizi.
Mtandao wa Facebook umekuwa maarufu duniani na tangu kuasisiwa kwake mwaka 2007, kwa sasa una wafuasi zaidi ya Bilioni moja ukitafsiriwa katika lugha 70.

Bernard James

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI