MAUAJI KIVU:BABA MTAKATIFU ATOA RAI



Baba Mtakatifu Fransisko ameligeukia jimbo la Kaskazini la Kivu katika taifa la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo jumatatu wakati wa maadhimisho ya kupalizwa Bikira Maria.
Jimbo la Mashariki kwa muda mrefu limekumbwa na vurugu zitokanazo na migogoro katika nchi za jirani ambapo mwisho wa juma watu wapatao 30 wameuawa.
“ Kwa malkia wa amani, ambaye tunamtafakari leo katika utukufu mbinguni, nataka kuaminisha tena juu ya wasiwasi na huzuni wa watu katika maeneo mengi duniani ambao ni wahanga wasio na hatia wa migogoro inayoendelea” Baba Mtakatifu amesema.
“ Fikra zangu zinaenda kwa watu wa Kivu Kaskazini, katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, ambao muda mfupi wameumizwa na mauaji ambayo kwa kipindi fulani yamekuwa yakifanywa katika ukimya wa aibu, bila kuvutia tahadhari zetu. Kwa bahati mbaya, wao ni sehemu ya watu wengi wasio na hatia ambao hawana uzito juu ya maoni ya dunia. ”
 “ Pengine Maria atapata kwa watu wote hisia za huruma na kuelewa na hamu ya amani na maelewano. "

Bernard James

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI