HURUMA NI NYENZO YA AMANI NA USHIRIKIANO

”Ilipokuwa jioni wanafunzi wake walimwendea wakamwambia,  hapa ni  nyikani, na sasa ni jioni,  basi uwaage watu  ili waende vijijini wakajinunulie chakula . Yesu akawaambia si lazima waende, wapeni nyingi Chakula .  Lakini wao wakamwambia wana mikate mitano na samaki wawili” Matayo 14: 13-21…… .
Aya hizo kutoka Injili ya Matayo , ziliongoza Katekesi  ya Jumatano ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mahujaji na wageni waliokusanyika katika ukumbi wa Paulo V1 wa Vatican. Papa  alitazama kwa kina muujiza  wa Yesu juu ya mikate mitano na samaki wawili.  Aidha Papa alitoa maelezo yaliyotangulia muujiza huu, ambamo Yesu anapokea habari za kifo cha Yohana Mbatizaji, na kuondoka  alipokuwa kwa njia ya mashua, akilenga kujitenga mbali na umati wa watu,   lakini watu hao walimfuata  huko  na akawaonea huruma,  na kuwaponya wagonjwa wao.  
Baba Mtakatifu ametafakari na kusema, tunaona kwamba, Yesu daima alikuwa,ni mtu wa huruma, daima aliwafikiria  wengine.Katika tukio hili tunaona kwamba alivutwa na hofu waliyokuwa nayo  watu, kubaki peke yao kama watelekezwa, licha kwamba yeye alikuwa ametiwa  simanzi na taarifa ya Kifo cha Yohana Mbatizaji, Nabii mwenye karama, aliyekuwa ametambua ukuu wa Yesu na kujiweka chini yake kama alivyosema, "Yeye ajaye baada yangu ana uwezo kuliko mimi" (Mt 3:11). Lakini  umati ulifuatana na Yesu kila mahali, kumsikiliza na kumpelekea wagonjwa ili aponye. . Papa aliongeza watu hao waliwaona ukuu wa Yesu, kwamba  ndiye kiongozi , na hakuwa na moyo wenye ubaridi  katika kuwapokea na kuwahudumia watu wengine.  Nao Umati wa watu haukutaka kuwa mbali naye kwa sababu walihitaji kuwa karibu nae , ingawa Yesu alihitaji kuwa katika hali ya faragha kwa ajili ya kutolea sala zake kwa Baba, kama maandishi mengi yanavyonyesha , Yesu mara nyingie nyakati za usiku alijitenga mahali pa faragha na kuomba kwa Baba yake.
Papa amesema kama ilivyokuwa wakati huo hata leo hii, Yesu ,  Mwalimu mwema, anaendelea kuyatolea maisha yake kwa watu. Huruma yake isiyoweza elezeka , inaonyesha kikamilifu jinsi anavyotaka kuwa karibu na watu , kukaa karibu na sisi na kutuokoa. Papa alieleza na kusisitiza Yesu anampenda sana kila mmoja wetu. Na anataka kuwa karibu nasi.
Katika fumbo la muujiza wa mikate na samaki wawili , tunaona jinsi Yesu anavyojali watu ilipokuwa jioni, Yesu anajali kulisha watu wale wote wenye uchovu na njaa.  Na ndivyo Yesu anavyojali kumhudumia kila anayemfuata, na anapenda kushirikisha mitume wake katika huduma ,kama alivyosema , wapeni ninyi chakula. Alipenda kuwaonyesha kwamba  mikate michache na samaki waliokuwa nao, kwa uwezo wa imani na maombi, inawezekana kuwalisha watu wote.  Hivyo huu ni muujiza wa  imani, maombi ,  huruma na upendo. Yesu "akamega mikate, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu" (v. 19).  Na hvyo ndivyo Bwana hukutana watu wahitaji kupitia watumishi wake na kumwezesha  kila mmoja wetu, ashiriki  kweli katika huruma yake.
Papa aliendelea kuizungumzia huruma ya Yesu akIsema , huruma yake na upendo wake daima  huwa ni  neema, husamehe dhambi, hudhihirisha kwamba, anatupenda  si katika hali ya nusunusu lakini kikamilifu.  Yesu huijaza mioyo yetu iliyopungikiwa kwa  upendo wake, msamaha wake na, huruma yake. Kwa hiyo, Yesu anaruhusu mitume wake kutekeleza amri yake ya Upendo. . Kwa njia hii wanajua njia ya kwenda: kulisha watu na kuwadumisha katika umoja ; yaani katika utumishi wa maisha na ushirika.
Papa alikamilisha katekesi na wito kwa Kanisa, akilitaka lidumu katika huduma na usharika ili kila muumini aweze kuwa daima chombo cha ushirika katika familia, kazini, Parokiani vikundini na jumuiya , kwa ishara inayoonekana ya huruma ya Mungu, ambayo haitaka mtu yeyote aondoke au kubaki katika upweke lakini katika  umoja wa watu na Mungu, na katika ushirika huu  kama  maishaya kila siku kwa kila mtu.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI