Wimbi la kuuawa kwa walinzi geita lamsononesha Askofu Kassala
WIMBI la
kuuawa mara kwa mara kwa walinzi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya mji
wa Geita yamemsononesha na kumtia simanzi Askofu Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki
la Geita.
Akizungumzia hali hiyo katika maadhimisho ya Misa maalum ya kutoa kutoa
Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Kuu la Jimbo la Bikira Maria Malkia wa
Amani ,alisema anasikitishwa kuona walinzi wakiendelea kuuawa kila wakati.
Alisema hali ya namna hiyo inaleta simanzi kubwa na pia ni
mshangao kwani pamoja na kuuawa kwa walinzi hao wauaji hakuna kitu
wanachochukua hali inayofanya watu watu kuyahusisha matukio hayo na imani za
kishirikina.
"Hali hii ya kuuawa kila siku kwa walinzi katika mji wetu wa
Geita si ishara nzuri hata kidogo na inashangaza hawa wanaohusika na mauaji
hayo hawachukui kitu chochote baada ya mauaji inatia shaka kuona imani za
kishirikina zikiendelea kushamiri kwa kiwango hiki" alisema Askofu
Kassala.
Hadi sasa jumla ya walinzi 20 wa makampuni mbalimbali za ulinzi na
walinzi binafsi wameuawa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Geita huku jeshi la
Polisi likishindwa kutoa majibu sahihi juu ya vifo hali inayowafanya wananchi
kubaki katika hali ya wasiwasi juu ya vitendo hivyo.
Askofu Kassala aliwahimiza waaamini hao na watu wengine kuacha
kudhani watapata nyota kwa kukatisha maisha ya wenzao akihimiza kutokubalika
kwa matendo hayo.
"Ndugu zangu wapendwa hivi kuhangaika kutafuta nyota kwa wale
ambao hawajaiona nyota? maana nyoya za waganga ni za muda na mtu ukihangaika na
kimwanga kidogo kinachokwisha muda mfupi giza litakapokuja utaongozwa na
nini?" alisema
Aliwahimiza waamini hao kuendelea kuwa na sifa za kuwa wafuasi wa
Kristo kwa matendo na mwenendo mwema huku akiwahiza sana kuwa daima na huruma
kwa wengine na kusameheana wanapokoseana.
Katika hatua nyingine Askofu Kassala aliwahimiza waamini
kujitahidi kufunga ndoa na kuacha visingizio vya kuchelewa kufunga ndoa kwa
kisingizio cha sherehe na kuendelea kujifungia masakramenti hali aliyosema
kiroho siyo jema.
Aidha alitoa wito kwa waamini na watu mbalimbali wa ndani na nje
ya Jimbo kujitokeza kukisaidia kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa huruma
kwani alisema gharama za kuwasomesha watoto hao zimekuwa kubwa na kulielemea
Jimbo.
Aliipongeza Parokia ya Bikira Maria wa Fatima kwa mchango wake
katika kituo hicho wakati wa Krismasi ambapo waamini wa Parokia hiy walichangia
jumla ya shilingi milioni saba za papo kwa papo ,huku akiihimiza na Parokia
hiyo ya Kanisa kuu kuweka mipango ya kusaidia kituo hicho.
Comments
Post a Comment