Ajali ya ndege: watu 37 wafariki dunia, nyumba 32 zawaka moto!

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa ajali ya Shirika la Ndege la Uturuki, Boing 747, ndege ya mizigo iliyoanguka Jumatatu tarehe 16 Januari 2017 na kusababisha watu zaidi ya 37 kufariki dunia na nyumba zaidi 32 kuungua kwa moto! Ajali hii imetokea umbali wa KM 30 kutoka katika Kiwanja cha Ndege cha Bishkek, nchini Kyrgztan.
Baba Mtakatifu katika salam za rambi rambi zilizoandikwa kwa niaba yake na  Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican anapenda kutoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu mzito kwa kuondokewa na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na makazi yao! Anamwomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma na mapendo, aweze kuwafariji majeruhi na kuwapokea marehemu kwenye raha na mwanga wa milele! Baba Mtakatifu anawatakia wananchi wote wa Kyrgzstan baraka na faraja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo!
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI