‘Kipaumbele cha Padri ni Ekaristi Takatifu’
PAROKO
wa Parokia ya Isimani Padri Leornad Maliva amewaasa mapadri kuangalia
vipaumbele vya utume wao hasa wanapopangiwa maeneo mapya ya kazi.
Padri Maliva ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Umoja wa Mapdri Jimbo Katoliki Iringa
(UMWAI) amesema, suala la msingi kwa padri yeyote anapopangiwa eneo jipya la
uchungaji ni uwepo wa Ekaristi Takatifu na sio umeme, barabara ya lami na
mitandao ya simu. Padri ahakikishe kuwa katika ratiba yake ya kila siku
anapanga muda wa kukaa na Yesu wa Ekaristi Takatifu.
“Padri hana sababu yeyote inayomfanya
akose muda wa kuabudu Ekaristi kila siku. Padre ni mwadhimishaji wa Ekaristi
Takatifu na ni vema aiabudu hata baada ya misa.
Katika sakramenti ya Ekaristi Takatifu,
Yesu ametuachia ukumbusho wa mateso yake ili mateso na mahangaiko yetu yapate
faraja katika kuiabudu hiyo Ekaristi.
Kwa padri, kuabudu Ekaristi takatifu ni
kielelezo cha unyenyekevu wa kukubali kuwa padre ni kiumbe dhaifu anayepata na
kuchota nguvu za utume wake katika ukumbusho wa mateso ya Yesu kwenye
sakramenti ya ajabu, yaani Ekaristi takatifu.
Padri Maliva ameyasema hayo katika
sherehe ya Jubilei ya miaka 25 kwa Padri Charles Muna, Br. Damian Wissa ambaye
ametiza miaka 25 ya utawa na Sista Maria Kasela (CST) aliyefunga nadhiri za
kwanza, sherehe ambazo zimefanyika katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata
parokia ya Kaning’ombe Jimbo Katoliki Iringa.
Ninafahamu mawasiliano katika ulimwengu
wa sasa ni jambo la msingi na muhimu lakini si kipaumbele kwa padri kwani
kipaumbele cha Padri ni Injili na
Ekaristi Takatifu. Network ni baada ya Injili na Ekaristi.
Inapendeza kuwasiliana na wengine na
kupata habari kama haki msingi ya mwanadamu lakini Padri asikatae, ama
kusononeka kupelekwa kwenye eneo la kazi ambako kuna changamoto za mtandao.
Suala la kwanza ni uwepo wa waamini,
Kanisa, Ekaristi Takatifu, Injili na mahitaji msingi ya mwanadamu kama malazi
na chakula ili aweze kuhudumia watu wa Mungu.
Tunaadhimisha miaka 100 ya Upadri na
miaka 150 ya Ukristo Tanzania Bara. Zipo changamoto mbalimbali a wamisionari wa
Kwanza amabo hawakuwa na mitandao, simu, magari na walikuta watu hawamju Kristo
wakaanza kuhubiri bila kukata tamaa hadi tumefika hapa tulipo leo.
Hivyo nasi katika changamoto zetu za
utandawazi, usitutoe nje ya utume wetu ukatufanya watumwa badala ya kuwa
watumwa wa Injili. “Ole wangu nisipoihubiri Injili.” Amesisitiza Padri Maliva.
Amesema kwamba haipendezi kwa mtumishi wa
Mungu kujali mambo ya dunia ambayo ki msingi hayana kipaumbele kwao.
“Wenzetu wanatukumbusha kushukuru Mungu
kwa wito tuliopewa kama zawadi kutoka kwake. Ni vyema tukawa na moyo wa shukrani na
kufurahia utume wetu,” amesisitiza Fr Maliva.
Awali Paroko waparokia hiyo Padri Charles
Mwipopo amesema kwamba wanamshukuru Mungu kwa kufikia sherehe hizo kwani mara
mbili wameihirisha kutoka na afya ya Padri Muna kutokuwa nzuri.
Misa hiyo iliongozwa na Pelate Monsinyori Julian Kangalawe na homilia imetolewa na Padri Maliva.
Comments
Post a Comment