Askofu Minde azidua Jubilei ya miaka 100 ya Upadri Kahama
ASKOFU
LUDOVICK Minde wa jimbo la Kahama amezindua rasmi Jubilee ya miaka 100 ya padri na kutoa wito kwa mapadri kuupenda na kuuenzi upadri wao ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Akihubiri
katika Misa Takatifu ya uzinduzi wa Jubilei hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Kanisa Kuu la jimbo la
Mtakatifu Karoli Lwanga Parokia ya Kahama mjini Askofu Minde amewasisitiza
mapadri kuutunza upadri kama lulu uweze
kuonekana katika utume wao kwa
Kanisa.
Aidha amewakubusha mapadri wajibu wao na
kuwataka kuendelea kuomba neema hiyo
ya kuupenda zaidi upadri , kuuenzi kwa sababu ni zawadi kuu ya
milele toka kwa Mungu
aliyowajalia ndani ya kanisa kwa
kushirikishwa ukuhani huo.
“Mapadri wanahitaji kuombewa katika utume
wao ili waweze kung’aa kama mwanga katika
dunia hii katika utumishi wao
wa uijilishaji kwa kumunganisha
mtu na mafumbo ya mbinguni wanapoazimisha misa .
Mapadri wameshirikishwa ukuhani huo kwa
mfano wa Melkisedeki Kuhani Mkuu na kutoa wito kwa waami kuwaombea kwa sala, kuwatunza, kuwasaidia,
kuwapenda na kuwapa ushirikiano waweze
kutimiza wajibu wao katika kumtumikia
Mungu kwenye maisha yao,”
amesisitiza.
Amesema kuwa, katika dunia ya sasa yenye
utandawazi mapadri na watawa wanakumbwa na changamoto mbalimbali hivyo ni rahisi kutoka
nje ya maisha yao na kufwata ya kidunia, hivyo amewataka waamini walei kuwasaidia mapadri na
watawa kuishi wito wao, waache kuwapotosha katika mambo mbalimbali ya
ulimwengu.
Wakati huohuo katika Jimbo la Kahama ,
Askofu Minde ameadhimisha Misa Takatifu ya kuweka Nadhili za Kwanza za Utawa
kwa Masista watatu wa shirika la Mabinti Masikini wa Bikira Maria iliyofanyika
katika Parokia ya Jina Takatifu la Yesu, Bukombe.
Askofu Minde amewataka wazazi na
walezi katika familia kuwaruhusu
watoto wanapokuwa na wito wa kumtumikia Mungu na kuwasaidia kufikia wito
huo.
“ Ndugu zangu wazazi waruhusuni watoto kujiunga
na maisha ya utawa pale Mungu anapowaita. Msiwachagulie miito kwani wito
unatoka kwa Mungu pekee,” amesisitiza Askofu Minde.
Aidha askofu Minde katika kazi zake za
kichungaji alitoa sakramenti ya kipaimara kwa watoto 581 wa Parokia ya Mtakatifu Stephano Shahidi na
kusisitiza umuhimu wa mafundisho ya Kanisa
Katoliki kwa watoto ili wawe wafuasi imara wa imani
kwa Yesu Kristo.
Comments
Post a Comment