Kilwa Chimbuko la Utawa Tanzania
KATIKA makala mojawapo niliwahi kuandika
kuwa wakristo wa kwanza Afrika Mashariki walibatizwa Kilwa. Historia ilionesha
kuwa Wareno walipofika Kilwa kisiwani kuanzia 1505 chini ya Francisco D’Almeida
na askari kama 500 waliitiisha Kilwa.
Wafransiskani
waliokuwepo kwenye meli hiyo walishuka wakaingia Kilwa Kisiwani wakasimika
msalaba na waliimba wimbo wa kumsifu Mungu yaani Te Deum. Kishapo askari wa
Kireno walishambulia Kilwa Kisiwani, waliiba na kuharibu mji.
Katika
mazingira hayo wananchi 40 waliomba kubatizwa na wakabatizwa. Kwa yeyote mwenye mawazo ya kihistoria
atajiuliza hao walikuwa ni akina nani na walitoka wapi? Maswali mengi yalibaki
kichwani mwangu.
Utafiti
wangu wa kihistoria umegundua kuwa Sultani wa kwanza wa Kilwa Kisiwani, Ali
Hasani Shiraz toka Uajemi kwenye miaka ya 960 hadi 1000 Mwaka wa Bwana aliweka
makao yake Kilwa Kisiwani. Mmoja kati ya wake zake alikuwa ni mama wa Ki
Ethiopia ambaye alikuwa mtumwa.
Historia
imegundua kuwa baadhi ya majina ya nasaba za masultani waliotawala Kilwa baada
ya Shiraz kufa kuanzia 1022 hadi 1499 yalikuwa na majina ya Kiyahudi kama vile
Ibrahimu, Suleiman na Dawudi. Hata
sultani wa mwisho kuondolewa na Wareno 1505 aliitwa Ibrahim Suleiman. Majina haya
yanaashiria aina ya ukristo wa Kiyahudi.
Tafiti
hizi zinathibitisha kuwa Yule Mama wa Ethiopia mtumwa huenda alikuwa ni mkristo
wa kanisa la Ethiopia ambalo katika kipindi hiki lilifikia kilele cha kiutawala
na walikuwa na koo zenye kudai nasaba ya Mfalme solomoni wa Yerusalem kuanzia
wakati wa koo za Kizagwe kwenye mika 1000 mwaka wa Bwana hadi 1974.
Duru
hizi zinathibitisha kabisa huko Kilwa Kisiwani kipindi hicho kulikuwa na
ukristo wenye asili ya kanisa la Ethiopia. Tusishangae sasa kwa nini wakati wa
Wareno watu 40 waliomba kubatizwa.
Mtafiti
mwingine mwenye asili ya Kifaransa aliyeanza utafiti wake 2009 amebaini kuwa
baadhi ya maandishi yaliyopatikana Kilwa
Kisiwani kwenye baadhi ya milango yanaashiria hapo Kilwa iliishi jumuiya ya
wakristo. Mtafiti huyo anadai kuwa hiyo
Jumuiya ilikuwa ni jumuiya ya kimonaki ambao huenda walitoka Siria.
Mtafiti
huyu, duru za kinasaba za Kilwa na wale waliobatizwa 40 wakati wa Ureno
vinathibitisha kuwa Kilwa Kisiwani kabla ya Wareno kulikuwa na Jumuiya wakristo.
Hivyo
ninaweza kusema pasina shaka Kilwa ni
chimbuko la Ukristo Tanzania. Kilwa ni chimbuko la Utawa na umonaki
Tanzania. Ni jambo la ajabu pia kabla ya
kuzaliwa kwa Ndanda na Peramiho 1931 eneo
lote liliitwa Jimbo la usimamizi
la kitume la Lindi. Tanzania sasa kuna monasteri
za akina Baba nne katika lilioitwa Jimbo la usimamizi la kitume la Lindi na
zaidi ya kumi ya mashirika ya masista.
Kilwa
ni chimbuko la umonaki Tanzania. Kanisa la Tanzania na hasa Jimbo la Lindi
kutafuta namna ya kuenzi Kilwa kama chimbuko la Ukristo Tanzania. Ni muhimu
sana tujifunze kwa kina Historia ya kanisa la Afrika. Kilwa ni sehemu muhimu
sana ya chimbuko la ukristu Tanzania.
0784306170
SIJAWAHI KUMUONA MWANDISHI MSHAWISHI MUONGO KAMA HUYU
ReplyDeleteALIEANDIKA MAKALA HII