TEC wapigwa msasa juu ya sheria ya ajira
WATUMISHI wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
wamepewa mafunzo maalum juu ya sheria ya kazi ili kuleta ufanisi katika
utendaji kazi ikiwa ni sehemu ya tekeleza sheria, timiza wajibu, na imarisha mahusiano chanya katika sehemu za kazi.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika katika Makao Makuu ya
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini jijini Dar es Salaam na
kuongozwa na wataalamu kutoka Wizara ya
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
wilaya ya Temeke.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
Padri Raymond Saba ameeleza kuwa, TEC imeamua kuwaalika wataalamu kutoka Wizara
ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu ili kutoa ufahamu wa sheria ya kazi na mahusiano kazini kwa lengo la
kuendesha taasisi katika utaratibu unaoleta ufanisi kwa kujenga mahusiano mazuri
yenye tija baina ya mwajiri na mwajiriwa.
“Lengo ni kuwasikiliza wataalamu wetu, tuwaelewe, tuzifahamu
na kuielewa sheria ya ajira ili kuweka mfumo wa utatuzi wa migogoro ya kazi kwa
njia ya usuluhishi, na uamuzi sahihi, kujenga mahusiano chanya na kupata
mwongozo wa kisheria kuhusu mahusiano mazuri mahala pa kazi na viwango vya
kazi,” amesema Padri Saba.
Akitoa ufafanuzi kuhusu sheria hiyo, Afisa Kazi mwandamizi
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wilaya ya Temeke Bi Vedastus
Kapongo ameeleza kuwa, kila mwajiriwa na mwajiri wana haki ya kuzijua sheria ya
kazi na mahusiano kazini Na.6/2004 ili kuwa na mfumo sahihi wa kuendesha
taasisi yoyote ile.
“Licha ya kuwa taasisi binafsi zina mamlaka ya kutunga
taratibu zake za kazi, taratibu hizo lazima zifuate mwongozo wa Sheria Mama ya
Ajira na mahusiano Kazini ya mwaka 2004 kwani hakuna aliye juu ya sheria, taratibu
na miongozo ya kazi katika sekta binafsi na zile za serikalini lazima
zisipingane na sheria hii kwani sheria hii ndiyo mwongozo wa nchi katika
ajira,” amesisitiza Bi. Kapongo.
Akifafanua juu ya matumizi ya sheria hiyo, Bi. Kapongo
ameeleza kuwa, Sheria hiyo inawahusu waajiri na wafanyakazi wote waliopo katika
sekta binafsi na umma Tanzania Bara lakini haiwahusu wafanyakazi walioajiriwa
katika utumishi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Jeshi la
Magereza na Jeshi la kujenga Taifa.
Kati ya vifungu vya sheria
alivyovifafanua ni pamoja na Ubaguzi katika ajira unaokatazwa chini ya kifungu
cha saba (7)
“Ubaguzi
hauruhusiwi katika mambo yafuatayo: Taratibu za ajira, Upandishwaji vyeo, Uhamisho,
Mafunzo, Mishahara, Mgawanyo wa majukumu, Kushusha cheo na Kuachisha kazi na
hatua za nidhamu.
Kwamba sheria inasema si ubaguzi
mwajiri kutoa ajira kulingana na Sifa au
mahitaji halisi ya kazi, Kulingana na Sheria ya Huduma za Ajira ya mwaka 1999, Kwa
upendeleo katika kukuza fursa sawa na kuondoa ubaguzi mhala pa kazi
(Affirmative action)”
Sheria ya mkataba
Amezungumzia pia sheria ya mkataba akisema kuwa, Mkataba ni
makubaliano ya pande mbili ikiwa na lengo la kutekeleza shughuli fulani ambapo
amebainisha kuwa mkataba huo lazima uwe wa hiari, umesainiwa na pande mbili zenye
akili timamu, lazima uwe na thamani,uwe wa maandishi wenye masharti
yanayoendana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004
Amezitaja aina za mikataba ya
Ajira kulingana na sheria hiyo akisema kuwa,
Saa za Kazi
Ameelezea pia sheria ya saa kazi
akisema kuwa, Sheria inaruhusu mfanyakazi afanye kazi
Siku 6 kwa wiki, Saa 45 kwa wiki na Saa 9 kwa siku.
Kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Sheria
ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6/2004 Mwajiri anawajibika kumpa angalau saa
moja ya kupumzika mfanyakazi aliyefanya kazi kwa masaa matano mfululizo kwa
siku.
Mwajiri hatakiwi kumfanyisha kazi mwajiriwa saa za ziada
bila kuwepo na makubaliano. Endapo mfanyakazi atakubaliana na mwajiri kufanya
kazi za ziada, saa za ziada hazitazidi masaa matatu kwa siku na masaa 50 kwa
wiki nne.
Malipo ya saa za ziada
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 (5) saa za ziada zitalipwa kwa
kiwango cha 1.5 ya mshahara wa saa kwa kila saa aliyofanya kazi mwajiriwa kwa
siku za kawaida.
Siku za mapumziko/sikukuu
Mfanyakazi anastahili kupumzika siku moja katika kila wiki
pamoja na siku zote za sikukuu. Pale ambapo kwa maridhiano na mwajiri, atafanya
kazi kwa siku za mapumziko atastahili kulipwa mara mbili ya mshahara wake kwa
kila saa atakayofanya kazi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha sheria ya Ajira na
Mahusiano Kazini, kwa makubaliano ya maandishi, mfanyakazi anaweza akafanya
kazi kwa masaa 12 kwa siku ikiwa ni pamoja na muda wa chakula cha mchana pasipo
kupata malipo ya ziada. Kwa mkataba huo mfanyakazi hatatakiwa kufanya kazi
zaidi ya Siku 5 kwa wiki, Saa 45 kwa wiki na Saa 10 kwa saa za ziada katika
wiki.
Kwa ufafanuzi zaidi
fuatilia gazeti la kiongozi katika matoleo yajayo ambapo sheria hii
itachapishwa mfululizo ili kuleta uelewa wa kina.
Comments
Post a Comment