Papa awatembelea waathirika wa tetemeko la ardhi Amatrice
Baba Mtakatifu Francisko amefanya ziara ya kushtukiza
katika maeneo yaliyokumbwa vibaya na tetemeko la aridhi , lililotokea
katika eneo la kati nchini Italia , tarehe 24Agosti 2016. Papa
amefanya ziara hii kama tendo la huruma, kwenda kukutana, kuwafariji na
kuonyesha mshikamano wake kwa waathirika, na hasa waliopoteza ndugu zao
na makazi yao kutokana na uharibifu mkubwa wa majengo hasa katika mji
wa Amatrice. Akiwa katika eneo hilo, Papa Francisko aliitembelea shule
ya msingi ya muda iliyoanzishwa katika eneo hilo kwa msaada wa kikosi
cha usalama wa raia cha Trento , na kisha akaenda karibu na eneo
lililoharibiwa vibaya zaidi, kujionea mwenyewe uhalibifu uliofanywa na
jenga hili, sehemu ambayo kwa sasa haruhusiwi mtu yeyote kuishi. Na pia
alipita katika eneo la Arquata del Tronto, Accumoli.
Katika eneo la shule ya msingi aliandamana na Askofu wa Rieti, Askofu Domenico Pompili, na alikutana na wanafunzi na walimu, na watoto wanafunzi bila kuchelea walimtumbuiza kwa nyimbo za kirafiki na kumpatia zawadi ya michoro yao ya kitoto, inayowakumbusha uwepo wa janga hili. Na kisha alitoa hotuba yake fupi, kwa watu waliokuwa wamemzunguka, ambamo aliwahakikishia ukaribu wake na kuwaomba pia wasimsahau katika sala zao.
Papa Francisko mara baada ya kupata taarifa za janga hili la tarehe 24 Agosti, Jumapili iliyofuatia wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 28 Agosti , ikiwa imepita siku nne baada ya tetemeko, alionyesha hamu yake ya kutaka kwenda kukutana na waathirika wa tetemeko , kama tendo la huruma. Kukutana na kuwapa maneno ya kuwafariji katika tumaini la Kikristo .
Na Jumapili iliyopita, wakati wa mkutano wa waandishi akirejea kutoka mjini Baku kwa ndege, Papa Francisko alisema, alirudia kuonyesha hamu yake ya kufanya ziara katika mazingira ya faragha, kuwatembelea wahanga wa tetemeko la aridhi katika mjiwa wa Amatrice, kama Padre, kama askofu na , kama Papa, bila msafara rasmi. Alipenda kuwa karibu na watu hao, hamu aliyoitimiza Jumanne hii.

Comments
Post a Comment