UKRISTO WAZIDI KUIMARIKA MAFIA
Zaidi ya watoto 800 wahiji na
kuacha historia kisiwani humo
10 waacha dini zao na kukubali
kubatizwa
“NENDENI
Mafia mkainjilishe. Kwa watoto wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam wanatambua
kwa nini huwa tunaenda Mafia kila mwaka. iIa ninyi wengine mtakaporudi
nitawaambia” hayo ni maneno ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akiwaaga watoto wa Utoto Mtakatifu
Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Ifakara na Mpanda katika viwanja vya Msimbazi
Centre, jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mafia.
Safari hiyo ilianza saa 1:42
asubuhi ikiongozwa na askari wa usalama barabarani, huku takribani watoto 800 wakiwa
wenye furaha wakiimba na kusali, na hatimaye waliwasili Mafia saa 11:30 jioni.
Watoto hao walipokelewa na Askofu
Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa pamoja
na Paroko wa Parokia ya Mafia Padri Francis Massawe.
“Mwanzoni mtu ukipangiwa kuja
Mafia iwe kwa shughuli ya kikazi au shughuli nyingine, unaona kama umeadhibiwa.
Tangu nchi hii ipate uhuru watu waliiona Mafia sio mahali pa kwenda. Kwa
kulitambua hilo Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akasema yeye atakwenda na
watoto wadogo kwa kuwa waliokuwa wanapanyanyapaa walikuwa ni watu wazima. Lakini
watoto ni wanyoofu, wasikivu, wanyenyekevu, na hawana hila mioyoni mwao” ameeleza
Askofu Nzigilwa
Akiongea na gazeti la Kiongozi
Padri Francis Massawe amesema kuwa Mafia ni kisiwa ambacho asilimia 90 ya
wakazi wake ni waislamu hivyo kina changamoto kubwa katika uinjilishaji, huku
akimuomba Kardinali Pengo azidi kuhamasisha vyama vingine vya kitume kwenda
kisiwani humo kuinjilisha kwani kuhiji kwao kunahamasisha waamini wengine
kubatiza watoto wao na kufunga ndoa.
Kutokana na Sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2013, idadi ya wakristo kisiwani humo ni 1693, ila hija ya
Utoto Mtakatifu kila mwaka imepelekea waislamu 10 kukubali kumpokea Kristo kwa
kubatizwa.
Geofrey
Hilmary, Mafia
Comments
Post a Comment