MALEZI IMARA:”MAWILI HAYA” ndio,ila wewe zaidi.
Lakini pia
tumesikia kauli za kutia moyo za watu waliofanikiwa na kudai kuwa ni kwa sababu
ya fulani nina maisha mazuri hivi, nisingemsikiliza ningeharibikiwa maisha.
Kauli
hizo hapo juu ni uthibitisho kuwa malezi imara ni matokeo ya muunganiko wa ushauri wanaotupatia watu
mbalimbali, athari za jamii inayotuzunguka na mwishowe lile mtu mwenyewe baada
ya kupokea hayo mawili analoona ni muhimu kulizingatia.
Mambo haya
matatu ni lazima yawekwe pamoja ili kumsaidia mtu kuwa na maamuzi bora na
mwishowe kuwa imara katika malezi yake. Kila jambo lina umuhimu wake.
Nafasi ya washauri:
Hawa
wanajumuisha wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zako wanaotumia nafasi walizonazo
kwako kukushauri la kufanya.
Hawa wana
umuhimu sana kwani waliokuzidi umri hukupatia yale yaliyowasaidia kuwa watu wa
heshima katika jamii walimo, ila wanakuepusha na mitego mibaya waliyowahi
kukutana nayo hivyo usije ingia huko.
Lakini swali
msingi hapa ni, Je ni kila litokalo kwa
washauri unalizingatia kama dira yako ya malezi bora? kisa tu aliyekuambia ni Baba au Mama yako au rafiki yako
ambaye hutaki kugombana naye hata siku moja.
Jamii:
Huchangia
pia katika makuzi yetu kimalezi.Kuna mifumo ya kijamii ambayo huna budi kuwa
nayo kama unataka kuwa mtu mwenye malezi bora, kwa mfano kushirikiana na
wenzako katika misiba na michango mbalimbali ya huduma za kijamii.
Ushauri wa
wanajamii pia ni mwingi la msingi ni hili tena, Je, kila linalofanyika kijijini
ni la kuzingatia? Je, kwa sababu michango ni muhimu utashiriki kuchangia kuleta
mganga wa kienyeji ili awatoe wachawi hasa jirani yako uliyekuwa unamhisi
hivyo?
Mawili haya sawa ila wewe mwenyewe
zaidi:
Ni katika
msingi huu kuwa si kila kitu wanachotoa washauri au kinachofanywa na jamii ni
cha kuzingatia.
Ni yale tu
mazuri ndiyo huwa tunayalenga ili yatusaidie kukua katika misingi imara ya
malezi.
Makundi hayo
hapo juu ni muhimu ila nafasi ya mtu binafsi ni ya muhimu zaidi katika kuwa na
malezi imara na endelevu. Kauli nyingi za wale ambao wamejikuta wakifuata
makundi haya bila kuwa na maamuzi yao binafsi zimekuwa daima, NAJUTA! SIKUJUA! NILISHAWISHIWA! NIKIMWONA
FULANI NATAMANI KUTAPIKA.
Majuto ni
mjukuu, daima uwe na sera ya “SAWA, ILA MIMI NAONA HIVI” yaani jitihada
binafsi kupokea ya washauri mbalimbali na jamii husika kisha upime na kufanya maamuzi yako mwenyewe lile ambalo kimsingi
litabaki kwako mwenyewe na hutamsingizia mtu.
Maisha ni
jinsi unavyoyatengeneza.
FR SAMUEL MVATI.
NDUNGU PARISH [SAME
DIOCESE]
Comments
Post a Comment