CARITAS TANZANIA INAVYOWASAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO
Mara baada ya kutokea kwa
tetemeko la ardhi Septemba 10, 2016 Idara ya Caritas Jimbo Katoliki Bukoba
ilifanya jitihada za makusudi za kutathmini madhara ya tetemeko hilo na kubaini
mahitaji yanayopaswa kupewa kipaumbele.
Katibu wa Caritas Jimbo
Katoliki Bukoba Padri Deogratius Mwikira, ameeleza kuwa ofisi yake imefanya
tathmini ya kubaini mahitaji ya haraka kwa wahanga wa tetemeko hilo.
Tathmini hiyo ilifanywa na jopo
la wana Caritas kwa kuzunguka nakutazama hali halisi, kufanya mahojiano ma
viongozi wa vijiji, dini, walimu wakuu na wakuu wa shule, na wawakilishi wa
vyama vya ushirika.
Tathmini hiyo imefanyika katika
vijiji vya Nyarugongo, Kiilima, karagala, Kigazi, Ruhano, Katolerwa na Minziro.
Vijiji vingine ni pamoja na Kabyaile, Katano, Bushaga, Ntungamo, Ibosa, Busimbe
B na Bugambakamo.
Tathmini hiyo imebaini
uharibifu wa shule 13, majengo ya dini 11, nyumba za watu wasiojiweza 2, Vituo
vya afya 3 na vyama vya ushirika vitatu.
Aidha watu waliofanyiwa
tathmini hiyo wameonyesha kukosa usalma kwa kuwa wanalala nje, kwenye baridi na
mali zao zikiwa nje.
Idadi
ya makazi
Idadi ya Kaya katika vijiji 14 vilivyofanyiwa
utafiti
|
5648
|
Kaya ziazoongozwa na wanawake
|
538
|
Kaya zenye walemavu
|
61
|
Kaya zinazoongozwa na watoto
|
91
|
Mtawanyiko
baada ya tetemeko
Wakazi wanaoishi/wahifadhi majirani zao
|
67
|
Waliohama makazi yao
|
495
|
Msaada
mpaka sasa
WALIOTOA
|
AINA YA MSAADA
|
ALIYEPOKEA
|
Serikali
|
Mablanketi, mashuka, biskuti, mchele,
maharage, sukari, ndoo
|
Walioathirika katika kijiji cha Minziro
|
Walioguswa
|
mashuka
|
Dispensari 1
|
Mahitaji
Msaada
unaohitajika
|
Wahusika
|
Mahema
|
Watoto, wazee, walemavu, wajane
|
Mablanketi
|
Watoto, wazee, walemavu, wajane
|
Mashuka
|
Watoto, wazee, walemavu, wajane
|
Saruji
|
Watoto, wazee, walemavu, wajane
|
Mabati
|
Watoto, wazee, walemavu, wajane
|
MSAADA
WA MFUKO WA MSAMARIA MWEMA KWA WALIOATHIRIKA NA TETEMEKO LA ARDHI
Kama ilivyo ada ya Kanisa
Katoliki, ifikapo Jumapili ya kwanza ya mwezi Septemba huadhimishwa Jumapili ya
Msamaria Mwema. Hapo katika parokia zote na vigango vyote vya Kanisa Katoliki
huhamasisha waamini kuchangia vitu na pesa kwa ajili ya watu wahitaji.
Kwa kutambua mahitaji ya
wahanga wa tetemeko la ardhi, Idara ya Caritas Bukoba iliamua kugawa mchango
uliotolewa katika jumapili ya msamaria mwema kwa waathirika wa tetemeko,
kupitia Kamati ya maafa ya mkoa chini ya uongozi wa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mustafa Kijuu.
Vitu vilivyotolewa ni kama
ifuatavyo:
Mashuka pea 100 Tsh 1,500,000
Nguo za watoto Tsh 93,400
Nguo za kike Tsh 1,460,000
Nguo za kiume Tsh 840, 0000
Viatu Tsh 265,000
Madaftari Tsh 530,000
Kalamu za wino Tsh 37,000
Kalamu ya risasi Tsh 10,000
Sabuni za miche Tsh 85,000
Sabuni za kuogea Tsh 6,500
Jumla Kuu Tsh 4,734,900
Baada
ya tathmini, CARITAS yawafariji waathirika wa tetemeko
BAADA ya kufanya tathmini ya madhara
yaliyoletwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mkoani Kagera, Idara
ya Caritas katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, imewafuta machozi
wahanga hao kwa kuwapelekea msaada wa vyakula vilivyosindikwa vyenye thamani ya
Tsh. Milioni 108.
Katibu Mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui |
Akiongea na Kiongozi ofisi
kwake, Katibu Mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui ameeleza kuwa msaada
huo wa vyakula vilivyosindikwa, ambavyo ni nyama na maharage, umewasilishwa kwa
Idara ya Caritas Jimbo Katoliki Bukoba, kwa ajili ya kupanga utaratibu unaofaa
wa kuwafikishia wahanga hao.
“Tumepeleka msaada wa tani 20
za vyakula vilivyosindikwa. Msaada huo utapelekwa kwa waathirika wa tetemeko la
ardhi, na watapewa kulingana na mahitaji yao. Idara ya Caritas Jimbo Katoliki
Bukoba itaratibu namna ya kuwafikia walengwa” ameeleza.
Licha ya msaada huo, caritas
imeshafanya tathmini ya kuzitambua familia zenye uhitaji maalum ili nao waweze
kupatiwa msaada kadiri ya mahitaji yao.
Ametaja familia hizo kuwa ni pamoja na zile za wajane, walemavu ambapo
watapatiwa vifaa vya nyumbani na vya ujenzi.
Comments
Post a Comment