MAKANISA YAENDELEA KUONGOZA UTOAJI HUDUMA ZA KIJAMII

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Kijamii (CSSC), Bw. Peter Maduki amesema katika sekta ya afya hadi kufikia Juni 2016, makanisa yalikuwa yanamiliki na kuendesha hospitali 102, vituo vya afya 102 na zahanati 696. “Kati ya hospitali 102, mbili ni za rufaa za kanda na 38 ni za hospitali teule za Halmashauri za Wilaya na hospitali nyingine 62 zinatoa huduma halmashauri mbalimbali,” amesema.
Amesema karibu asilimia 38 ya hospitali hapa nchini zinamilikiwa na makanisa na nyingi ziko maeneo ya vijijini. Pia alisema kuna chuo kikuu kimoja, vyuo vikuu vishiriki vitatu, na vyuo vya mafunzo ya kati 62 ambavyo vinatoa kozi za uuguzi, maabara na ufamasia.

Kuhusu sekta ya elimu, Bw. Maduki amesema makanisa yanatoa elimu kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hadi kufikia Juni, 2016, makanisa yalikuwa na shuke za msingi 161, za sekondari 369, na vyuo vya ufundi stadi 126. “Pia tuna vyuo vya ualimu 14, vyuo vikuu tisa, vyuo vikuu vishiriki 17 na vituo vya vyuo vikuu saba,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI