BODI YA MIKOPO: TAARIFA MAHUSUSI

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekamilisha zoezi la kurekebisha fomu za maombi ya mikopo kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Zoezi hilo lilianza tarehe 3 na kumalizika tarehe 7 Oktoba 2016.
 

Kwa sasa Bodi inaendelea na hatua za awali za upangaji wa mikopo ambapo taarifa za wanafunzi watakaopangiwa mikopo zitatolewa kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz siku chache zijazo.
 
NB: Bodi inawakumbusha waombaji mikopo wote kuwa makini na watu wasio waaminifu wanaoweza kutumia fursa hii kujipatia fedha isivyo halali.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI