Posts

Showing posts from August, 2016

MAMA TEREZA KUTANGAZWA MTAKATIFU TAREHE 4 SEPTEMBA

Image
Pichani siku ya jumapili, Juni 29, 1997 Papa John Paul II akimsalimu Mama Tereza wa Kalkutta walipokutana huko St. Peter Basilica Vatican. Mama Tereza atatangazwa Mtakatifu Sept. 4 2016. Mama Tereza alijitoa kwa moyo mkubwa kuwasaidia masikini huku akizingatia misingi ya kanisa katoliki hasa kuwa na moyo wa huruma.

JIMBO KATOLIKI BUNDA LAPATA PADRI MPYA, KATIKA PAROKIA YA NAKAMWA KISIWANI UKEREWE

Image
Jimbo katoliki Bunda limempata padri mpya, Joanes Nyawach katika misa takatifu ya upadrisho iliyofanyika katika parokia ya Nakamwa Kisiwani Ukerewe na kuongozwa na Baba Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo hilo. Yafuatayo ni baadhi ya matukio muhimu yaliyotokea siku hiyo.  

INDONESIA: SHAMBULIZI LA KIGAIDI LASHINDWA KANISANI,PADRI AJERUHIWA

Image
Ingeweza kuwa kama ilivyotokea nchi Ufaransa hivi karibuni, nchini Indonesia katika kanisa la Mtakatifu Joseph mjini Medan, mvamizi mmoja akiwa na kisu ameingia katika misa ya jumapili akijaribu kumdhuru Padri na waamini waliokuwemo kanisani. Kwa mujibu wa mashuhuda, hili limekuwa ni shambulio la kigaidi, likilenga kulipua bomu katika mkusanyiko kanisani, lakini hakukuwa na wahanga. Kwa mujibu wa mashuhuda, mlipuaji wa bomu alikaa kati ya waamini wakati alipojaribu kulipua bomu la kienyeji, ambalo lililipuka kinyume na makusudio ya mlipuaji. Huku kajeruhiwa, mlipuaji aliweza kumfikia Padri Albert Pandianga(60)   na kumjeruhi kwa kisu. Jeshi la polisi lilifika mapema eneo la tukio na kulidhibiti. Viashiria vya kundi la Islamic State ikiwemo alama yao vimekutwa katika vitu vilivyoachwa na mlipuaji. Indonesia ni taifa lenye waamini wengi wa dini ya kiislamu kuliko taifa lolote ulimwenguni. Hata hivyo kumekuwepo na baadhi ya makundi yenye msimamo mkali mengine yakiung...

MAGAZETINI LEO JUMATANO AUGUST 31

Image

MBINGA: WATANZANIA WATAKIWA KUDUMISHA TUNU ZA UMOJA NA AMANI

Image
                                            Watanzania wameshauriwa kudumisha umoja na mshikamano uliopo ili tunu ya amani iliyopo katika nchi iweze kudumu. Hayo yamesemwa hivi karibuni   na Padre Christian Mhagama wakati akihubiri katika misa takatifu ya jubilee ya mapadri 11 wa jimbo la Mbinga katika kanisa kuu la Mtakatifu Kilian jimboni Mbinga. Padre Christian amesema kuwa,” haitoshi kuimba tu kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani pasipo kuienzi mifumo ya umoja na mshikamano iliyowekwa na waasisi wetu.” Amesema migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafugaji   inaashiria kupoteza tunu hiyo ya amani na kuiweka Tanzania kuonekana kwa ndani   kuwa sio kisiwa cha amani. Aidha   amewataka mapadri hao kumi na moja {11} kuulinda umoja walioudhamiria kuufuata ...

TANZIA: MAMA MKUU WA KWANZA WA SHIRIKA LA MT. AGNES CHIPOLE AFARIKI DUNIA

Image
Waamini wametakiwa kutokata tamaa wanapopatwa na magonjwa, dhiki, mateso na misiba katika maisha. Hayo yamesemwa hivi karibuni na Padre Camilius Haule naibu wa Askofu mkuu wa jimbo kuu Katoliki Songea wakati wa adhimisho la misa takatifu ya mazishi ya Sista Ester Mwali OSB aliyekuwa mama mkuu wa kwanza wa shirika la Mtakatifu Agnes Chipole. Padre Camilius amesema kuwa,” tunaguswa na mateso na misiba kwa sababu sisi ni binadamu tunaonja maumivu, na mateso kwa sababu kifo hakizoeleki na mtu yoyote kati yetu”.  Amesema kutokana na hali hiyo waamini hawana budi kushikamana na Mungu ili wapate nguvu ya kumwendea Yesu kwa pamoja.  Amesema  Mungu ndiye anayejua kwa nini ametuumba na kutupa uzima na kuutwaa tena na Mungu peke yake ndiye mwenye uwezo wa kumrejeshea mtu maisha yake tena kama alivyofanya kwa kumfufua Lazaro. Padre Camilius amesema, “imani yetu itufanye tuamini kuwa, mateso na misiba  tunayopata hapa duniani yatufanye tutambue kwamba tunapomaliza ...

PAPA ATETA NA MUASISI WA FACEBOOK

Image
Papa Fransisi amekutana na muasisi na mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg pamoja na mkewe Priscilla Chan katika mkutano wa faragha uliofanyika kwenye makazi ya Papa huko Casa Santa Marta Vatican. Waraka uliotolewa na ofisi ya habari ya Vatican umesema Papa na muasisi huyo wamejadili namna ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano kuondoa umaskini, kuhamasisha utamaduni wa makutano, na kusaidia kufikisha ujumbe wa matumaini, hususani kwa watu wasio na usaidizi. Mtandao wa Facebook umekuwa maarufu duniani na tangu kuasisiwa kwake mwaka 2007, kwa sasa una wafuasi zaidi ya Bilioni moja ukitafsiriwa katika lugha 70. Bernard James