TANZANIA INTERFAITH PARTNERSHIP KUUTOKOMEZA UKIMWI
Tanzania Interfaith Partnership(TIP) shirika linalojumuisha taasisi za dini Tanzania yaani Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristu Tanzania (CCT), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), na Ofisi ya Mufti Zanzibar (MOZ) limefanya kikao huku lengo kubwa likiwa ni kuweka mkakati wa pamoja wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi,kuboresha maelewano baina ya dini zote,kuboresha amani na mshikamano uliopo nchini.
Taasisi hizi zilianza kushirikiana mwaka 2002 chini ya Balma in Gilead ambalo ni Shirika la Kimarekani.
Pamoja na mambo mengine,kikao hiki kimejadili namna ya kutoa huduma za afya hasa za kupambana na Maambukizi ya UKIMWI na UKIMWi wenyewe.
Mkakati huu unaohusisha mikoa ya Kigoma, Manyara na Mara unalenga zaidi,watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,huduma za wagonjwa nyumbani, ushauri nasaha na upimaji VVU kwa hiari, na kinga dhidi ya UKIMWI.
Kikao hiki kimehudhuriwa na wakuu wote wa taasisi za dini kama ifuatavyo: Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa (Raisi – TEC), Askofu Mkuu Alex Malasusa (Mwenyekiti – CCT), Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi (BAKWATA), na Sheikh Saleh Omar Kaabi (Mufti Zanzizar). Pia kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu wote wa Taasisi hizi: Padri Raymond Saba (TEC),John Mapesa Kaimu Katibu Mkuu CCT, Sheikh Seleman Lolila (BAKWATA), na Sheikh Fadhil Suleiman Soraga (MoZ).
Wajumbe wa mkutano huo wamebainisha kuwa licha ya TIP kuwa Mkombozi mkuu kwa watu wote
hasa katika sekta ya afya,ni vema ikafanya
tathmini kwa yale yaliyokwisha kufanyika yaani miaka mitano na kuona wapi ilipata changamoto na kuweka mikakati ya kurekebisha na kuboresha na pale ilipofanikiwa kuendeleza na kujenga misingi mizuri zaidi.
Kwa pamoja wajumbe hao wamepongeza juhudi zinazofanywa na Sekretariati ya TIP na kubainisha kuwa endapo ikitumika vizuri,basi pamoja na mambo ya afya TIP inaweza kuwa sehemu nzuri ya kuongelea masuala ya mapatano ya dini mbalimbali(interfaith forum).
Katika kutekeleza
shughuli zake TIP na Balm in Gilead zimekuwa zikipata ufadhili kutoka kwa
Shirika la Kimarekani linaloitwa Center for Disease Control (CDC).
TEC
Comments
Post a Comment