Hongera Dkt. Magufuli kwa kudumisha maadili na utawala wa sheria!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli |
Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi wa Jimbo Kuu la Mwanza,
anaipongeza Serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania kwa kujikita katika
kanuni maadili, maendeleo na utawala wa sheria katika mapambano dhidi rushwa na
ufisadi wa mali ya umma, saratani ambayo ilikuwa imeifikisha Tanzania mahali
pabaya katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa!
Haya yameelezwa na Askofu mkuu Ruwaichi katika mahojiano maalum
na gazeti la Daily News linalochapishwa nchini Tanzania. Askofu mkuu
Ruwaichi anaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika
mchakato wa maboresho ya maisha ya watanzania, sanjari na kujikita katika
kanunu maadili, utawala wa sheria na heshima ya binadamu. Jitihada za Serikali
katika kukusanya kodi zinapaswa kuungwa mkono, ili kuimarisha uchumi na
kuondokana na tabia ya kuwa na uchumi tegemezi kwa wahisani wa nje.
Askofu mkuu Ruwaichi anakaza kusema, mchango wa wafadhili kutoka
nje, utasaidia mchakato wa maboresho ya maisha ya watanzania wengi, hususan
wanaoishi vijijini, kwa kuwa na uhakika wa umeme ili kukoleza shughuli za
uzalishaji na huduma; pamoja na kuendelea kuboresha huduma za elimu na afya;
mambo ambayo yanawagusa watanzania wa kawaida!
Askofu Mkuu Ruwaichi anaendelea
kumpongeza Rais Magufulu na Serikali yake na kuwataka kukaza uzi ili Tanzania
iweze kuheshimika kutokana na utawala wa sheria, kanuni maadili na maendeleo
kwa watu wake. Mambo haya si tu kwa ajili ya watumishi wa serikali, bali
watanzania wote katika ujumla wao, wanapaswa kufuata sheria na kanuni maadili.
Kutokana na udhibiti wa ukusanyaji kodi, Pato Ghafi la Taifa, GNP limeongezeka
kwa asilia 7% katika miezi ya hivi karibuni!
Comments
Post a Comment