Papa amteua Padri Kassala kuwa Askofu mpya Jimbo la Geita
Baba
Mtakatifu Fransisko amemteua Padri Flavian Kassala kuwa askofu mpya wa Jimbo
Katoliki Geita.
Taarifa iliyotolewa na Katibu
Mkuu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba kwa vyombo
vya habari imeeleza kuwa Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko
Padilla anayo furaha kutangaza kuwa Papa Fransisko amemteua Padri Kassala kuwa
Askofu mpya wa Jimbo la Geita.
Mpaka wakati wa uteuzi wake
Askofu mteule Kassala alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella
Maris Mtwara.
Askofu mteule Kassala
amezaliwa Desemba 4, 1967 katika Parokia ya Sumve, Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.
Alipata masomo yake ya Sekondari katika Seminari ndogo ya Mtakatifu Pio wa X,
iliyoko Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma.
Alijiendeleza zaidi kwenye
Seminari Ndogo ya Sanu Jimbo Katoliki Mbulu. Masomo ya falsafa aliyapata kutoka
Seminari ya Mtakatifu Anthony wa Padua- Ntungamo, iliyoko Jimbo Katoliki la
Bukoba.
Askofu mteule Kassala
alijipatia elimu ya Teolojia kwenye Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo- Kipalapala
iliyoko Jimbo Kuu Katoliki Tabora.
Alipewa Daraja Takatifu la
Upadri hapo Julai 11, 1999 kama Padri wa Jimbo Katoliki Geita. Baada ya
Upadrisho kati ya mwaka 1999 hadi mwaka 2002 alikuwa ni Paroko msaidizi katika
Parokia ya Sengerema, Jimbo Katoliki la Geita.
Mwaka 2002- 2004 alikuwa ni
mlezi na Padri wa maisha ya kiroho Seminari ndogo ya Bikira Maria Malkia wa
Mitume, Jimbo Katoliki Geita pamoja na kuwa Mkurugenzi wa Jimbo kwa Mashirika
ya Kimissionari ya Kipapa.
Kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka
2012 alitumwa na Jimbo kujiendeleza zaidi katika utume wa vijana na katekesi
katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Wasalesiani, kilichoko mjini Roma na hapo
akajipatia shahada ya uzamivu.
Mwaka 2013 Askofu
mteule Kassala alirejea Jimboni Geita na huko akapewa dhamana ya kuratibu
miradi ya Jimbo. Kuanzia mwaka 2013- 2015 akepewa dhamana ya kusimamia na
kufundisha Chuo Kikuu cha SAUT, Kitivo cha Utalii, Arusha.
Mwaka 2015 alihamishiwa
katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris.
Itakumbuka
kwamba, Jimbo Katoliki Geita limekuwa wazi kuanzia Machi 14, 2014 baada ya Baba
Mtakatifu Fransisko kumhamisha na kumpandisha hadhi Askofu Mkuu Damian Dallu
kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Songea
To God be the Glory and Honor AMEN!
ReplyDelete