BALOZI WA BABA MTAKATIFU NCHINI ASKOFU MKUU FRANSISKO PADILLA AKITABARUKU KANISA JIPYA JIMBO KATOLIKI KAHAMA
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akiweka jiwe la msingi katika jengo la masomo ya TEHAMA katika shule ya wasichana ya Mtakatifu Theresia wa Avilla Jimbo Katoliki Kahama katika ziara yake ya kichungaji ya siku tano jimboni humo (Picha na Patrick Mabula)
Kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima
Watoto wa shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu wa Yesu wakiongoza maandamano siku ya kutabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima jimbo la Kahama (Picha na Patrick Mabula)
Padri Andrew Maziku akiwa amebeba masalia ya Watakatifu ya kuzikwa kwenye Altare wakati wa maandamano ya kuelekea kanisa jipya la Ekaristi Takatifu -Kabuhima jimbo la Kahama wakati wa misa ya kutabaruku kanisa hilo (Picha na Patrick Mabula)
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akikata utepe kufungua kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima Jimbo Katoliki Kahama lenye uwezo wa kuingiza waamini zaidi ya 1,500 kwa mara moja (Picha na Patrick Mabula)
Paroko wa Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima Padri Salvatore Guerrera akifungua rasmi mlango wa kanisa jipya baada ya kupewa ufungua na Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla baada ya kukata utepe (Picha na Patrick Mabula)
Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akizika masalia ya Watakatifu katika Altare ya Kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima jimbo la Kahama alipolibariki na kulitabaruku. Katikati ni Askofu wa Jimbo la Kahama Mhashamu Ludovick Minde na kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo Padri Salvatore Guerrera (Picha na Patrick Mabula)
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akipaka mafuta matakatifu ya Krisma katika Altare alipokuwa akitabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima, kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo Padri Salvatore Guerrera (Picha na Patrick Mabula)
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Fransisko Padilla akiweka ubani kwenye karai yenye mkaaa juu ya altare alipokuwa akitabaruku kanisa jipya la Parokia ya Ekaristi Takatifu -Kabuhima Jimbo Katoliki Kahama. Pembeni yake ni Askofu Ludovick Minde wa jimbo la Kahama (Picha na Patrick Mabula)
Comments
Post a Comment