Mahakama ya Kanisa Katoliki
Historia
fupi ya uanzishwaji wake.
Mambo
karibu yote unayoyaona katika Kanisa yana asili yake ama katika Biblia,
Mafundisho ya Mababa wenye mamlaka katika Kanisa (Magisterium), au mapokeo ya
Kanisa (Tradition).
BibliaTakatifu
1Kor
6:1-6
Anathubutuje
mmoja wenu kumshtaki ndugu muumini mbele ya mahakama ya watu wasiomjua Mungu
badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu ? .....Aibu kwenu! Ndiyo kusema
hakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekima kiasi cha kuweza kutatua tatizo
kati ya ndugu waumini? Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu
yake mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini.
Mwaka
197, Baba wa Kanisa Tertullian akiandika kuwatetea wakristo waliokuwa wanateswa,
(apology) anawakumbusha watawala wa
Kirumi waliokuwa wanawatesa wakristo tena kwa kusingiziwa tu, kwamba watu hawa
ni wema tena wana mahakama zao nzuri wanaamua mambo yao vizuri ambayo ninyi
yanawaletea magomvi. Anawashauri waige mfumo wa mahakama zao ambazo ni nzuri.
Didascalia ni mkusanyo wa mafundisho ya mitume inaeleza
kurasa baada ya kurasa kwamba kuhusu mfumo wa mahakama ya wakristu. Inamtaja
askofu kama Hakimu mkuu wa kundi lake alilokabidhiwa na jinsi anavyotakiwa
kuendesha kesi ya mtu aliyesingiziwa, jinsi ambavyo hatakiwi kupokea rushwa, asiwe na upendeleo
kwa watu wenye kipato na asidharau wala kuwaonea maskini katika maamuzi yake.
Kwa
kifupi mahakama za Kanisa zina historia ndefu toka kwenye Maandiko Matakatifu,
mapokeo ya Kanisa mpaka leo kwenye Kitabu cha Sheria za Kanisa (Code of Canon
Law 1983).
Kwanini
mahakama ndani ya Kanisa:
Kanisa
ni jumuiya ya wabatizwa chini wa uongozi wa wachungaji wao. Kwenye ngazi ya
jimbo mchungaji wake ni askofu wa jimbo.
Kumbe jumuiya yoyote ile inahitaji sheria ili iishi vizuri. Hebu fikiria
kama kusingekuwa na sheria za barabarani kwa sababu wote ni wakristu na
wataendesha magari kikristu, kuna ambao wangebaki masaa mengi barabarani.
Kumbe
jumuiya yoyote isiyokuwa na sheria itaishia kuwa na fujo tu. Kitakachotawala
hapo ni (life of the Jungle, survival of the fittest). Kuna hatari wa wenye
nguvu kukanyaga haki za wanyonge na kuwajeruhi wengine.
Mambo
yanayoshughulikiwa na mahakama za Kanisa
Kanisa
lina haki ya kutoa maamuzi (hukumu) kwa mashauri(kesi) zinahusu masuala ya
kiroho au pale sheria za Kanisa zinapokiukwa. Maamuzi haya yanatolewa kupitia
ngazi mbalimbali za mahakama za Kanisa.
Mahakama hizi zinaitwa Tribunals. Kuna mashauri mengi yanayoshughulikiwa
na mahakama hizi ila nyingi zilizopa hapa nchini zinashughulikia sana masuala
ya ndoa.
Watu
wanaleta maombi yao kwenye mahakama hizi ili mahakama ichunguze uhalali au
ubatili wa ndoa zao ambazo zimekumbwa na matatizo na labda kuishi tena pamoja
haiwezekani. Ndio maana wengi wanaziita
mahakama hizi kuwa ni mahakama za kesi za ndoa.
Ngazi za mahakama za Kanisa.
1. Mahakama ya mwanzo
Kila
jimbo linatakiwa liwe na mahakama yake ya mwanzo kisheria. Askofu wa jimbo
husika ndiye hakimu mkuu wa mahakama hiyo. Lakini kwa kuwa askofu ana kazi
nyingi za kichungaji basi kwa kawaida anawachagua mahakimu kadhaa ambao
wataongozwa na hakimu kiongozi anayeitwa Judicial vicar (wakili wa Askofu
upande wa sheria).
Anatakiwa
awe Mkleri (padri) mwenye Licentiate (masters) au (Ph. D) katika sheria za
Kanisa. Na katika jimbo letu la Tanga, mimi ndiye Judicial vicar. Kutokana na
uhaba wa wataalamu wa sheria za Kanisa, baadhi ya majimbo yanaungana na kufanya
mahakama moja ya kimajimbo, na maaskofu wa majimbo hayo wanamchagua mmoja wao
awe ndiye hakimu mkuu na mwangalizi wa mahakama hiyo.
Mahakama
hii inaweza kuwa na mahakimu wengi, na wahudumu wengine wa mahakama kadiri ya
sheria za Kanisa, au inaweza kuwa ya hakimu mmoja na msaidizi wake, chini ya
Askofu wa jimbo ambaye ndiye anabaki kuwa hakimu na hao wahudumu ni wasaidizi
wake tu.
Fahamu, muundo na kazi zake
2. Mahakama ya rufaa, mahakama
ya Jimbo Kuu
Mahakama
ya mwanzo inapokea kesi kutoka katika jimbo husika na wanazifanyia mchakato wa
kufikia maamuzi (process), na wakishatoa hukumu yao, hawaruhusiwi kutangaza
hukumu hiyo kwa wahusika mpaka ipelekwe mahakama ya ngazi ya pili, kwa mfano
hapa kwetu Tanga tunapeleka Dar es Salaam kwa sababu jimbo la Tanga liko chini
ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Sasa
kule Dar es Salaam mahakimu nao wanaipitia ile kesi iliyotoka kwenye mahakama
ya mwanzo na kama hukumu yao itawiana na
hukumu iliyotoka mahakama ya mwanzo basi
kesi itakuwa imekwisha na hukumu hiyo watakabidhiwa wahusika.
3. Mahakama
ya Rufaa Roman Rota
Hii
ni mahakama ya rufaa ngazi ya tatu, iko chini ya Baba Mtakatifu. Inapokea rufaa za kesi kutoka mahakama ngazi
ya pili. Pia inashughulikia kesi ambazo haziwezi kufanywa katika mahakama za
ngazi ya kwanza na ya pili. Kwamfano kesi zinahusu wakuu wa mashirika ya
kitawa, au kesi za maraisi wa nchi, nk.
4. Mahakama nyingine: Apostolic Signatura na
Apostolic Penitentiary.
Mahakama
ya Apostolic Signatura, ni mahakama ya juu kabisa katika kanisa la Roma. Ina
shughulika na kesi ambazo zimewakilishwa kwa Baba Mtakatifu mwenyewe na yeye
anateua makardinali watano kuifanya kwa niaba yake.
Ila
ni kesi nadra sana za namna hii. Mahakama ya Apostolic Penitentiary
inajihusisha na masuala ya ndani, yaani internal forum. Zote mbili zinafanya
kazi kwa niaba ya Baba Mtakatifu.
Comments
Post a Comment