HURUMA NI UFUNGUO WA MLANGO WA KUMFIKIA MUNGU-PAPA FRANCIS
Wajumbe wa Mkutano wa 38 wa Kitaifa wa Caritas Italiana, hivi karibuni wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko. Papa katika hotuba yake amekazia zaidi umuhimu wa kazi waliyokabidhiwa na kanisa tangu wakati wa kuanzishwa kwake mwaka 1972, katika kuhamaisha kanisa mahalia na wamini binafsi katika kuona maana na wajibu muhimu kutoa huduma na msada kwa watu wahitaji katika nyakati hizi zetu. Papa amewahimiza kama ilivyokuwa siku za nyuma hata leo hii, katika uaminifu wa hisia mpya na uwajibikaji, wanaendelea kutembea katika njia mpya na ubunifu kwa ajili ya kukabiliana na pia uhakiki unaolenga kuimarisha na kutoa maelekezo yaliyo bora zaidi katika yale yaliyokwisha fanyika tangu kuanzishwa kwake na jinsi ya kuyaendeleza.
Hivyo Papa ametaja kwamba utume wao umejikita katika elimu, ambamo ni lengo la Caritas la siku zote katika ushirika wa Kanisa na huduma katika mapana yake , lenye kudai dhamira ya upendo thabiti kwa kilabinadamu, na hasa katika kutoa kipaumbele kwa maskini ,kama Yesu alivyofundisha , kutoa msaada na kwa jirani na hasa wahitaji zaidi (Mat 25.35-40). Upendo unaopaswa uonekane katika hatua zote za utendaji wa Caritas na ishara zinazowakilisha mfano asilia wa kazi za ufundishaji za Caritas katika ngazi zote. Papa alieleza na kuhimiza ufundishaji kwa vitendo, na hasa katika lengo la kusaidia maskini kukua katika utu na jamii ya Kikristo kutembea katika nyayo za Kristo pamoja na vyama vya kiraia, kwa uangalifu kukubali wajibu wao , kama Papa Benedikto XVI alivyosema katika hotuba yake kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia miaka 40 ya Caritas Italia, 24 Novemba 2011.
Aidha Hotuba ya Papa Francisko imegusia changamoto na utata wa wakati wetu, unaofanya kazi za Caritas kuwa ngumu katika kutoa msaada wake muhimu kimatendo, na katika kuhakikisha kuwa ni huduma ya hisani inayodhamiriwa kwa kila mtu, yaani, kwamba jumuiya zote za Kikristo kuwa walimu wa upendo, ili jamii nzima iweze kuchochewa kukua katika upendo wenye kutafuta njia mpya za kuwa karibu na maskini wengi, uwezo wa kusoma na kukabiliana na hali ngumu na madhulumu yanayofanywa kwa mamilioni ya watu si nchini Italia, Ulaya peke yake lakini dunaini kote. Papa ameendelea kuwataka Wakristo kupitia chombo hiki cha Caritas, wawe kichocheo muhimu katika ujenzi wa uhusiano mzuri na taasisi za kiraia na uwepo wa sheria muafaka katika neema ya manufaa na utetezi wa makundi ya watu wanaoishi katika mazingira magumu zaidi.
Aidha Papa alitazama dhamira ya upendo kwa jirani akiwaelekea wakimbizi na wahamiaji. Tatizo la wahamiaji ambalo leo hii linawasilisha kipeo halisi kinachohitaji uwepo wa sera hai zenye kuona mbali zawadi ya utajiri unaoandamana na wahamiaji na wakimbizi. Kwa hiyo Papa amehimiza Caritas kuwa na ubunifu mpya kwa ajili ya ujenzi wa mshikamano ulio thabti zaidi kati ya wakazi wa Italia na wageni , na uwepo wa mwendelezo msingi wa utamaduni na ujuzi sahihi wa wataalamu , katika utatuzi wa mambo yanayoweza leta utata fulani au kuwa na sura ya kipekee.
Papa alikamilisha hotuba yake kwa kuhimiza Caritas kutenda kwa ujasiri kamili mbele ya uso wa Kristo Mfufuka na kwa ujasiri unaotoka kwa Roho Mtakatifu wenye kuwawezesha kusonga mbele bila woga na kugundua mitazamo mipya ya Maaskofu , na uimarishaji wa mfumo na motisha,inayoweza kutoa jibu lenye ufanisi zaidi kwa Bwana, anayeonekana katika nyuso za wahitaji, wake kwa waume. Papa alieleza na kuziweka kazi kwa Kanisa za Caritas nchini ya maombezi ya Bikira Maria, na Mwenye Heri Paulo Paul VI. Kwao wote aliwapa baraka zake za Kipapa na kuwaomba pia wamwombee.
Mkutano huu wa Caritas Italiana , umefanyika kwa muda wa siku tatu mfululizo , 18-21 Aprili 2016, katika jengo la Fraterna Domus la Sacrofano Roma, ikiwa ni Mkutano wa 38 wa Kitaifa, ukiongozwa na Madakuu” Kuweni na Huruma kama Baba yenu alivyo na Huruma ( Lk 6, 36). Mada hii iliyolenga moja kwa moja katika maadhmisho ya Jubilee ya mwaka Mtakatifu wa Huruma kama ilivyotangazwa na Papa Francisko kwamba: neno Huruma ni ufunguo wa mlango wa kumfikia Mungu kati yetu na katika kuwafikia wengine hasa wanaoishi katika hali ngumu za kukata tamaa na waliosaulika pembezoni katika maisha ya kijami.
Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka matawi yote 220 ya Caritas Italia ,pia kama sehemu ya kusherehekea miaka 45 tangu kuanzishwa kwake, na kama jukwaa la kupima utendaji wa kazi za kichungaji katika huduma ya watu maskini na kanisa nchini Italia, na katika mtazamo wa kutembea pamoja hata kwa siku za baadaye katika mwanga wa Waraka wa Kitume wa "Injili ya Furaha" na Mwaka wa Jubilee ya Huruma na Waraka wa" Laudato Si".
Comments
Post a Comment