MUHIMU SANA
JE UNALIJUA SHIRIKA LA MASISTA WA UPENDO?
Shirika hili lilianzishwa mwaka 1950,mwanziilishi wa shirika
hili ni Mwenyeheri mama Terezia wa Calcutta.Shirika hili linaongozwa na karama
ya Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani.Pia kufanya kazi kwa ajili ya ukombozi
wa Roho za watu.
Shirika hili linaongozwa na karama ya watu ya kukidhi kiu
ya milele ya Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani.Pia kufanya kazi kwa ajili
ya ukombozi wa Roho za watu.
Shirika hili limesambaa sana Duniani, masista hawa
wanafanya kazi katika mabara na nchi zifuatazo:India,Amerika yote ya
kaskazini,Amerika ya kati,Amerika ya kusini,Mashariki ya kati, Afrika ya
kaskazini,Afrika Magharibi,Afrika ya kati,Afrika ya kusini,Misri,Libya,Morocco,
Algeria,Tunisia,Sudani,Djibuti,Uhabeshi,Kenya,Tanzania,SieraLeone,Liberia,Kameruni,Benini,Nigeria,Gambia,Burkina
Faso na Mali.
Masista pia wapo katika nchi ya Afrika, Uganda, Burundi,
Rwanda, Chad, Afrika kusini, Msumbiji, Congo , Kongo (DRC), Malawi, Niger,
Ivory Coast, Zimbabwe, Zambia, Mauritius, Visiwa vya Ushelisheli, Madagascar.
Tuone
pia katika bara la Ulaya.
Masista
wanafanya kazi katika nchi za Uingereza, Ireland, Iceland, Denmark, Ujerumani,
Ubeligiji, Uholanzi, Swideni, Norway, Austria, Uswizi , Malta, Uhispania,
Ureno,Ufaransa, Ugririki, Italia, Albania, Yugoslavia, Macedonia, Groatia,
Slovenia, Poland, Rumania, Hungary, Bulgaria, Slovakia, Ekistan,Chekislovakia,
Lithuania, Estonia, Latvia,Finland,Urusi, Ukraine, Belorusia, Georgia, Armenia,
Tajikistan,Uzbekistan, Kazakhstan, Syria, Iraki, Jordan, Lebanon, palestina,
Israeli, Yemen, Mashariki ya mbali , Ufilipino, Singapore, Thailand,, Mongolia,
Uchina, Cambodia, Japani,Taiwani Korea, Australia, New Zealand, Papua
Ginea,(PNG).
Kwa
ujumla Masista hawa wapo kwenye mabara 5, nchi 130 duniani, na wananyumba zao
720 duniani,
Je
unafahamu Masharti ya kujiunga na shirika la Masista wa Upendo au wa Huruma?
Ili
msichana ajiunge na Shirika la Masista wa Upendo hana budi kuwa na sifa
zifuatazo;
1). Binti
awe amehitimu kidato cha nne.
2). Binti
awe na cheti kinacholingana na kidato cha nne kinachotambulika na serikali.
3). Atoke
katika familia nzuri ya kikatoliki.
4). Awe
na afya njema ya kimaumbile, kiakili na kiroho.
5). Awe
na umri kuanzia (18-24) katika nchi za Afrika.
6). Kijana
awe na moyo wa umisionari
Tuone
changamoto wanazo kumbana nazo:
Kushuka
kwa miito, vijana wengi wanapenda kazi za mishahara,baadhi ya wazazi wanapenda kuoza
watoto wao na kupata mahari kama vile ng’ombe 100.Changamoto nyingine ni muda
mrefu wa malezi wa miaka minne hivyo wanakata tamaa upesi na kuondoka.
Jumla
ya Masista ni, 5,340, wanovisi 60, wapostolanti 50.
Kwa
wanaopenda kujiunga na shirika la Masista wa upendo anaweza tuma barua yake
kupitia anuani ifuatavyo.
Mkurugenzi
wa Miito
Box
858
Tabora.
Na.
Thomas Mambo - Tabora
Comments
Post a Comment