Mtakatifu Gemma Galgani
Alipata neema ya kupata Madonda Matakatifu
Mtakatifu Gemma Galgani
|
GEMMA Galgani
alizaliwa Machi 12, 1878 kwenye kijiji kidogo cha Tuskan karibu na Lucca,
alikuwa mmoja kati ya watu ambao Mungu mara kwa mara alimchagua kuwa shahidi
maalumu wa Mateso ya Yesu , ambapo aliweza kuyapata.
Baba
yake alikuwa mkemia na mtu mzuri sana, mama yake pia alikuwa mwanamke
mtakatifu. Familia yao walikuwa nane ambapo Gemma yeye alikuwa mtoto wanne, akiwa na umri wa miaka
saba Gemma alifiwa na mama yake mzazi.
Ilikuwa katika mafundisho ya mwanzo kabisa
Gemma aliweza kuwa na uchaji wa mateso ya bwana. Katika umri wa miaka tisa alipata Komunio ya
Kwanza, alishindwa kueleza namna gani alivyoshindwa kujieleza kipindi hicho
alichounganika kati ya roho yake na Bwana.
Gemma
alipenda ukimya na upweke na alikuwa
mara nyingi sio muongeaji. Usichana wake ulitawaliwa na kuteseka kwa mambo
mbalimbali kama vile majaribu ya ndani, vilevile ugonjwa ambapo ulisababisha
hata daktari kumkataza kurudi tena shuleni mwaka 1894, pia hali mbaya ya
kiuchumi ya ndugu zake, madharau ya watu waliomcheka kutokana na mazoea yake ya
kidini.
Gemma
alitamani sana kuwa mtawa, lakini alikataliwa mara mbili na Wakuu wa Mashirika
mawili tofauti ya kitawa kwa kigezo cha afya yake mbaya. Pamoja na hayo aliweza
kuishi maisha ya sala na kiroho sana kama mkristo mlei. Siku moja baada ya
kukomunika, Bwana Yesu alimtokea na kusema naye; “Gemma ninakutarajia kalvari.”
Mawazo, maneno na matendo yake yalimwelekea Yesu tu. “Alimwambia Bwana
utakapotaka kunitesa, tusifanye kelele, bali mambo yote yawe siri. Mimi nataka
kukupenda kwa msalaba wako. Sitaki kitu kingine ila kimoja tu : nataka kukupenda”.
Baada
ya maumivu ya ugonjwa muda mrefu aliweka nadhiri ya usafi wa moyo na ilipokuwa
februari 1899 alijiunga na Novena ya Mtakatifu Margareth Mary.
Mtakatifu
Gabrieli alimtokea na kumuahidi kufanya novena pamoja naye. Walifanya novena
hiyo kila siku usiku, akisali pamoja naye. Aliipeleka kwa baba yake wa kiroho,
alipokea komunyo na Rose akiwa kitandani na hatimaye kupona kabisa.
Muda
mfupi baada ya kupona ugonjwa wake, alitaka kuwa mtawa katika Shirika la
Passonist lakini afya yake haikumruhusu.
Siku
ya mkesha wa sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu mwaka 1899, akisaidiwa na
malaika wake mlinzi na Mama yetu Bikira
Maria, Gemma alipata toka kwa Bwana Madonda Matakatifu na yalikuwa yanamtokea
kila Alhamisi jioni hadi siku ya ijumaa mchana.
Mapadri
wa passionisti walimsaidia kama washauri wake wa kiroho. Yalitokea mara kwa
mara miaka 1899 na 1901 yalikuwa yakichuruzika damu nyingi sana na
kumsababishia maumivu makali mno, hata gemma alikuwa akidhani atazimia roho.
Alipata
maono, ufunuo, na maunganiko yalikuwa mara kwa mara, na alizungumza mara kwa
mara na Malaika wake mlinzi aliyemuona na pia aliweza kuwa na zawadi ya unabii
na ufahamu usio wa kawaida sifa za utakatifu wake zilienea nje na fadhila nyingi zilipatikana kupitia sala
zake.
Alifariki
Aprili 11 1903 akiwa na miaka ishirini na tano, alipojitoa mwenyewe kama sadaka
kwa wenye dhambi hasa kwa mapadri wenye mapungufu. Kabla ya kufikia miaka
arobaini alitangazwa Mtakatifu na Papa Pio XII siku ya sikukuu ya kupaa kwa
Bwana 2 Mei mwaka 1940.
Imetayarishwa na
Padri wa shirika la Karmeli, Paroko Msaidizi Parokia ya Mtakatifu Theresia wa
Mtoto Yesu, Mbezi Mwisho na Mkurugenzi wa Miito. Kwa msaada wa vitibu vya,
Saint Companions for Each Day, Oxford Dictionary of saints, Maisha ya
watakatifu. 0764038597, theoocd@gmail.com
Hakika historia ya Mtakatifu Gemma imenigusa sana na kunipa faraja kuu sababu mama yangu anaitwa Gemma na alikuwa mtu wa sala pia alipata mateso ya kuumwa kupararazi hata kushindwa kutembea kwa miaka 5 baada tu ya baba yangu kufariki. Na katika kuumwa kwake aliishikiria imani na hata ugonjwa wake ulituimarisha kama familia na hata kifo chase Mungu mwema aliweza nionyesha na kunipa nguvu na mguso mkubwa wa kumshukuru MUNGU kuliko lawama na hata baada ya kifo chake MUNGU mwema alituangazia nuru ya yale yaliyokuwa yanatupa huzuni. Sasa hii inanipa nguvu ya kuona jina la Gemma lina nguvu katika kristo na mama ameungana na Gemma akiwa nae ni mtakatifu na muombezi wetu.
ReplyDeleteHongera fr.
ReplyDeletehakika ni historia nzuri sanna na inafundisha
ReplyDeleteAsante fr.
ReplyDelete