Mjue Mtakatifu Peter wa Verona shahidi
Mjue Mtakatifu Peter wa Verona shahidi
Alipingana
na mafundisho ya uwongo toka utoto wake
MTAKATIFU Peter alizaliwa Verona mwaka
1205. Wazazi wake walikuwa watu wenye kupinga mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Hata hivyo wazazi wake walimpeleka katika shule ya Katoiliki kwa sababu
kulikuwa hakuna shule nyingine katika jiji hilo isipokuwa shule ya katoliki.
Mara
alijifunza si kwa kusoma na kuandika pia hata nasadiki. Toka
utoto wake alipinga mafundisho ya uwongo
Siku moja, wakati anakaribia
miaka saba alipokuwa anakuja toka
shuleni alikutana na mjomba wake aliyekuwa mpinga mafundisho ya Kanisa Katoliki
alimuuliza nini alichojifunza. Mvulana huyu alimjibu,
nimejifunza kanuni ya imani “nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba
mbingu na dunia”.
Hivyo ndivyo alivyomjibu mjomba
wake, na mjomba wake akamwambia hii si sawa
na alimsisitiza aache kuamini kuhusu hili. Lakini Peter alikataa
kupotoshwa na maneno ya kudhihaki ya kudharau vitu vitakatifu. Mjomba wake
baada ya kugundua kuwa mwanae huyu anapingana na mafundisho ya uwongo aliamua
kutompeleka tena kusoma katika shule ya kikatoliki.
Hata
hivyo baba yake aliamua kumpeleka Bologna kuendelea na masomo. Pale alikuwa na
nafasi ya kusoma vitabu vya kikatoliki ambavyo vilimsaidia kuongeza ufahamu
wake na kumuimarisha katika imani yake. Katika mji huu alifahamiana na
mtakatifu Dominiki mwazilishi wa wadominikani, na alimuomba ili aweze
kumuingiza katika jumuiya yake mpya aliyoanzisha.
Ombi
lake lilikubaliwa na aliguswa na maisha ya ndani ya kiroho, kwa kipindi kifupi
alikuwa mfano wa kila fadhila. Baada ya kumaliza masomo na kupadirishwa,
alichaguliwa kuhubiri na aliichukulia
kazi hii kwa mafanikio mazuri na
alijulikana katika Italia yote kwa jina la mtume.
Siku
moja alipokuwa katika katika sala, alikuwa amezama ndani zaidi katika sala,
mara mabikira watatu na mashahidi walimtokea, walikuwa Mtakatifu Agnes,
Catherine, Cecilia, waliongea naye kama binadamu mwingine anavyozungumza na
wenzake, mtawa mmoja bila kufikiria
alipita alisikia walichoongea na kwenda kutoa taarifa kwa Baba mkuu wa
nyumba kwamba Peter amewaingiza wanawake katika chumba chake.
Baba
mkuu bila hata kudadisi alichukulia taarifa hii kama kashfa ndogo, alimuita
Peter mbele ya wenzake na kumwambia kuhusu kitendo hicho kama kashfa. Peter
alikuwa mnyenyekevu kueleza au kuzifunulia neema ambazo alizopata toka
mbinguni, huku akipiga magoti, na
“kusema mimi ni mwenye dhambi na Nipo tayari kupokea adhabu”.
Haya
maneno yalichukuliwa kama kama ni ukweli aliokubali toka kwa mashataka
aliyopata toka kwa ndugu zake na alipewa adhabu kwenda kwenye Konventi nyingine
na kuwekwa kama mfungwa na kutopewa nafasi ya kuhubiri au kukutana na mtu
yeyote. Pamoja na kutokewa na kuongea na watakatifu hao, na pia kwa kushtumiwa
na ndugu wenzake yeye alikubali adhabu hiyo kwa unyenyekevu na hata
hajalalamika lakini kwa uvumilivu alikuwa na tumaini kwamba ipo siku kwa muda
wake Mungu atamfunulia.
Siku
moja alijilaza kifudifudi na kulia mbele ya msalaba na kusema, “O, Mungu wangu kwanini kitu hakijulikani
bado kwa mtu asiye na hatia? Baada ya hapo alisikia sauti ikimwambia, jifunze
toka kwangu kwa unyenyekevu kuvumilia msalaba uzito ambao huwezi kuulinganisha
na wangu”.
Baada
ya kusikia maneno hayo alijazwa na furaha na kuamini kwamba hana kitu chochote
zaidi bali kuteseka kwa ajili ya Kristo.
Kwa
muda mrefu Mungu alimletea mwanga mtu wake asiye na hatia kwa ndugu zake ambao
walimshutumu na hatimaye alipokelewa na kuanza upya kazi yake ya mwanzo na
kuendelea kuhubiri kwenye sehemu mbalimbali za mji na vijijini Mpaka kifo chake.
Aliwabadilisha wenye dhambi wengi na
wengi wale waliokuwa wanapinga mafundisho ya kanisa na kuhufahamu ukweli.
Wakati
wa miaka mingi ya kufanya kazi yake ya kuhubiri, Mungu alimfunulia kwamba kifo chake kipo karibu na kitakuwa
kama alivyotamani. Siku moja watu waliokuwa wawili ambao walikuwa wameazimwa na
watu wasioamini mafundisho ya kanisa walimtegea sehemu ambayo alikuwa anapita ili
wamdhuru kwenye kichaka.
Walimpiga
kichwani na upanga mara nyingi. Chini ya ardhi alichovya kidole chake kwenye damu
zilizokuwa zinamtoka na kuandika kwenye udongo. “Nasadiki kwa Mungu Baba” na
kuinua macho yake juu na kusema “mikononi mwako bwana naiweka Roho yangu”. Na
kufariki. Wale wauaji waliondoka huku walimchoma katika moyo wake.
Mwili
wake ulizikwa katika kanisa la Mt.Eustorgius. Miujiza mingi ilifanyika na
ilimpelekea Papa Innocent IV kumtangaza mtakatifu.
Imetayarishw
na padre. Theophil. C.Wabukundi, OCD. Wa
Shirika la Karmeli, Paroko Msaidi Parokia ya Mt. Theresia wa mtoto Yesu Mbezi Mwisho, na Mkurugenzi wa Miito. 0764038597, theoocd@gmail.com
I wishes to joined in your carmelite congregation father
ReplyDelete