Waraka mwingine wa Papa Fransisko kutolewa Aprili 8
Waraka mwingine wa Baba Mtakatifu Fransisko juu
ya Sinodi ya Familia unatarajiwa kutolewa siku ya Ijumaa Aprili 8, huku waraka huo
ukipewa jina la “Amoris Laetitia”, yaani
“Furaha ya upendo”
Waraka huo utatolewa rasmi na Katibu Mkuu wa
Sinodi ya Maaskofu Kardinali Lorenzo Baldisseri, na Askofu Mkuu wa Vienna
Kardinali Christoph Schönborn.
Miongoni mwa watu watakaohudhuria tukio hilo ni
pamoja na wanandoa Prof. Francesco Miano, ambaye ni Mhadhiri wa Falsafa katika
Chuo Kikuu cha Roma (Tor Vergata), na Prof. Giuseppina De Simone.
Itakumbukwa kuwa hapo mwaka jana Katibu Mkuu wa
Vatikani Kardinali Pietro Parolin alisema kuwa Waraka huu wa Papa utakuwa
unajikita katika kuhitimisha Sinodi, kama ilivyo utamaduni wake.
Sinodi juu ya familia iliyofanyika kwa takribani
wiki 3 iliwakutanisha Maaskofu 270 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu utume wa
familia na changamoto zake.
Comments
Post a Comment