Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Kupaa Bwana, Mbinguni, tarehe 25 Mei 2017, alikutana na kuzungumza na wakleri pamoja na watawa wa Jimbo Katoliki la Bata, huko Equatorial Guinea kwa kukazia utambulisho wao kama Kanisa familia ya Mungu inayowajibika, dhana iliyotiliwa mkazo sana katika maadhimisho ya Sinodi ya kwanza ya Maaskofu kwa ajili ya Kanisa la Afrika. Huu ni mwaliko wa kuendelea pia kushikamana na Kanisa la kiulimwengu katika mchakato mzima wa uinjilishaji, lakini kwa namna ya pekee na Askofu wao Juan Matogo Oyama. Kardinali Filoni anawapongeza wakleri na watawa kuwa mchakato mzima wa uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa huduma makini katika sekta ya elimu, afya, ustawi na maendeleo endelevu ya watu wa Mungu nchini Equatorial Guinea: dhamana, utume na asili ya Kanisa ambalo linatumwa na Kristo Yesu ili kuinjilisha. Uinjilishaji ni sehemu ya vinasaba vya maisha, utume na changamoto ...