Zaidi ya Vijana 6,000 wanufaika na mafunzo ya maadili Arusha
|
ZAIDI ya vijana wakatoliki elfu sitini (6000) wa Jimbo Kuu
Katoliki Arusha wamenufaika na elimu ya malezi
na maadili mema ambayo itawawezesha wawe na utu na kuboresha mbegu bora
katika familia.
Hayo yamesemwa na
Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu alipokuwa
akizungumza katika maadhimisho ya sherehe ya upadrisho wa mapadri watatu
zilizofanyika katika parokia ya Burka Arusha.
Askofu Lebulu
amebainisha kuwa Jimbo hilo linapenda kuwaandaa viongozi wakiwa wadogo kupitia
shule za pekee za Seminari za Jimbo hilo ikiwemo ya Usa River ambayo ni kwa
ajili ya wavulana pamoja na ya Seminari iliyopo Kisongo ambayo ni ya kuwaandaa
wasichana ili waweze kukua katika maadili mema.
Amefafanua kuwa
vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinazidi kushamiri katika jamii kutokana na
wazazi kushindwa kusimamia malezi ya watoto na kwamba Kanisa Katoliki
limejiwekea utaratibu wa kuelimisha vijana ambao wamemaliza darasa la saba ili
kuwajengea maadili ambayo yatawajenga katika utu na hatimaye kuwezesha familia
kujua.
Padri Fulgence
Mallya ambaye ni Mkurugenzi wa Miito wa Jimbo hilo amesema kuwa kupatikana kwa
mapadri hao ni neema kwani awali ilikuwa changamoto na kwamba wataweza
kulisaidia Kanisa Katoliki kufikia watu wengi na kuwapatia huduma.
Amesema kuwa Jimbo
hilo limekaa miaka mitano bila kupata watumishi na kwamba kufanikiwa kupata mapadri watatu katika Jimbo kutasaidia Parokia kuongezeka na kupata wahudumu pia
kuweza kuwafikia watu wanaohitaji huduma katika jamii tofauti na ilivyokuwa
hapo awali.
“Jimbo letu limekaa
muda wa miaka mutano bila kupata mapadri wapya, hivyo naamini mapadri hawa
wataweza kuhudumia parokia zetu lakini hata kuweza kuhudumia watu kwani watu
nao wanazidi kuongezeka lakini watenda kazi ni wachache zaidi,” Amesema.
Aidha amesema kuwa
wakristo wanapaswa kuendelea kusali kumwomba Mungu ili zile mbegu ya wito zinazosiwa na Mungu katika familia ziendelee kukua na hatimaye
waendelee kupata mapadri ambao watawezesha
kubadilisha ulimwengu kuwa na maadili mema.
Amewataja mapadri
waliopewa daraja hilo kuwa ni pamoja na padri Alfred Fadhili (anakwenda
kutumika Seminari ndogo ya Jimbo Oldonyosambu), padri Kariuki Ndege (anakwenda
Parokia ya Kijungu Wilaya ya Kiteto)
na padri Emanueli Swai
(amepangiwa Seminari ya matayarisho User River ya Mtakatifu Kaloli Rwanga).
Comments
Post a Comment