Jeshi la Polisi latakiwa kumkamata mtuhumiwa wa ubakaji
BAadhi
ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wameliomba Jeshi la Polisi mkoani hapa kudhibiti
vitendo vya uhalifu wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara.
Hatua hii imekuja baada ya
mfanyabiashara wa mtaa wa Swaswa Kata ya Ipagala Manispaa ya Dodoma Charles
Kalinga maarufu kama Chaz Pub mwenye umri wa miaka 43 kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa
miaka 17 wa kidato cha nne katika Shule
ya Sekondari ya Dodoma.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni
majira ya saa moja usiku katika mtaa huo wa Swaswa baada ya mtoto huyo kusikika
akipiga kelele akiwa katika pagale ambapo mama wa mtoto na majirani walimkuta
mtuhumiwa akiwa amemlalia mtoto huyo huku akiwa ameshamuingilia kimwili.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wenzake,
Bi Devota Metusela amesema wamechoshwa na vitendo hivyo vinavyojirudia na
kusababisha hofu kwa jamii.
“Kwa kweli hali hii inatuchosha mpaka
wakati mwingine tunakosa imani na Jeshi la Polisi,” Anasema.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi
wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt Caroline Damiani amethibitisha
kumpokea mwanafunzi huyo ambaye anadaiwa kubakwa ambapo alikuwa na hali mbaya.
Pia Dkt Caroline amesema
wamempokea mgonjwa Charles Kalinga
ambaye anashukiwa juu ya ubakaji huo akiwa na majeraha ambapo ametibiwa na
kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Naye Balozi wa Mtaa wa Kidongochekundu,
Rojas Mtunya amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kufanya vitendo
vya ubakaji mara kwa mara na hivyo kuliomba jeshi la polisi kutenda haki.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
kuwa Dodoma siyo salama kwa wahalifu na hivyo lazima sheria ichukue mkondo
wake.
Comments
Post a Comment