Askofu Maluma-Upadri ni kujitoa bila kubakiza
Mapadri
nchini wametakiwa kujitoa kwa hiyari yao bila kujibakiza katika maisha yao ya
utume wa kipadri ndani ya Kanisa ili kuisaidia jamii hasa ya kitanzania
kuondokana na matendo maovu ambayo yanajitokeza kila kukicha.
Hayo
yamesemwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Alfred Maluma alipokuwa
akihubiri katika Kanisa Kuu la Mt. Yosefu jimboni humo katika adhimisho la Misa
Takatifu ya watakatifu Petro na Paulo Mitume, ambapo yalitolewa madaraja ya
Upadri na Ushemasi.
Aliyepata
Daraja Takatifu ya Upadri siku ni Shemasi Jimsoni Mtifu wa Shirika la Mapendo
la Warosiminiani-Tanga na waliopata Daraja la Ushemasi na Waseminari ni Frank
Mwinami na JohnBosco Mligo wa Jimbo Katoliki Njombe.
Comments
Post a Comment