Wakristo waaswa kujinyenyekeza ili kufanikiwa
WITO
umetolewa kwa Wakristo wote nchini kuisikiliza sauti ya Mungu na kulisoma neno lake pamoja na kulitendea
kazi kwenye maisha yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na
kujinyenyekeza mbele za Mungu ili waweze kupokea baraka, amani pamoja na
mafanikio.
Wito huo
umetolewa na Padri Severien Olesanare Yoshila wa Jimbo Kuu Arusha katika Parokia ya Mtakatifu.Mathias
Ngaramtoni, hivi karibuni katika mahubiri yake kanisani hapo.
“Ni lazima
kukubali kunyenyekea mbele za Mungu na kuisikiliza sauti yake kila
wakati ili kuweza kutembea kwenye ulinzi
wake. Kutosikiliza sauti ya Mungu au kutokuwa mnyenyekevu
kumekuwa kukileta madhara makubwa kwa
mwanadamu ikiwa ni pamoja na kukosa ulinzi wa Mungu.Pia lazima kutambua
sauti ya Mungu inacho tafuta kwa mwanadamu ni
kumfanikisha na kumpa ulinzi utakaomsaidia mwanadamu kutembea kwenye
nguvu za Mungu siku zote.” Amesema
Ameongeza ‘’Watu wengi
wamekuwa wakishindwa kupokea
baraka za Mungu kutokana na wao kushindwa kupata muda wa kulisoma neno na
kulitafakari, lazima mwamini ukubali
kufanya kazi kwa bidii na kumpenda Mungu ili uone baraka na mafanikio
yadumuyo.”
Padri,Severien
amesema Neema ya Mungu humuwezesha mwanadamu kupokea baraka pamoja na mafanikio
huku Mungu akiachilia milango ya baraka pale anapopataka.
Aidha amesisitiza
‘’Lazima watu wapambane kwa kufanya kazi kwa bidii na kumpenda Mungu ili waone
baraka zake na mafanikio yadumuyo maishani. Na unapotamani kupata mafanikio lazima utamani kwanza
kuongozwa na Mungu, kuwa mnyenyekevu na
kufanya kazi kwa bidii.”
Comments
Post a Comment