‘Waliopata ujauzito shuleni wabuni njia mpya ya maisha
MKurugenzi wa
Utume wa Walei Jimbo Katoliki Kigoma Padri John Mbivilila amempongeza Rais John
Pombe Magufuli kwa kuliwekea mkazo suala la wanafunzi kutokuendelea kusoma
katika shule za Serikali pindi
wanapopata ujauzito wakiwa shuleni.
Ameyasema
hayo wakati akizungumza na gazeti hili ambapo amesema kauli ya Rais Magufuli
imekuja kwa wakati muafaka maana Taifa lilikuwa linamomonyoka kimaadili kwa
kasi.
“Ukiwaacha
waendelee kuzaa halafu warudi shuleni tafsiri yake umeruhusu waendelee kufanya
uasherati jambo ambalo ni marufuku kwani
hudumaza maendeleo ya taaluma nchini,” Amesema padri Mbivilila.
Aidha
padri Mbivilila amesema kuwa ni kweli wapo wanafunzi hubakwa wakiwa katika umri
mdogo ila ni wachache sana ukilinganisha na takwimu ya wanaopata mimba kwa
kujitakia, hivyo ni vyema Rais aungwe mkono katika hili ili kupunguza mimba
mashuleni.
“Ukimpeleka
shule wakati huohuo akiwa na mtoto sasa anaenda kufanya nini kama siyo kupata
ujauzito mwingine, kwa kweli lazima kuwepo utaratibu maalumu wakukabiliana na
aibu ya namna hiyo kwa Taifa letu,” amesema padri Mbivilila.
Hata hivyo
amesema kuwa zamani watoto walikuwa na maadili mazuri kutokana na malezi mazuri
ambapo sasa hivi imekuwa tofauti,
mwanafunzi kupata ujauzito imekuwa jambo la kawaida hali ambayo siyo nzuri
kimtazamo.
Padri
Mbivilila ameongeza kuwa kama mwanafunzi kapendekeza kuzaa basi aendelee na
utaratibu huohuo kuliko kurudi shuleni kupata mimba tena na kuwasababishia
wazazi gharama zisizo na msingi.
Comments
Post a Comment