Parokia ya Mtakatifu Anna, iliyoko ndani ya Vatican, Jumatano, tarehe 26 Julai 2017 imeadhimisha kumbu kumbu ya Watakatifu Yoakim na Anna, wazazi wake Bikira Maria kwa kusali kwa ajili ya kuombea maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana, yatakayotimua vumbi kuanzia mwezi Oktoba, 2018 hapa mjini Vatican kwa kuongozwa na kauli mbiu “Vijana, Imani na Mang’amuzi ya Miito”. Waamini wamesali pia kwa ajili ya kuombea maadhimisho ya Siku ya XXXIV ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2019 yatakayoadhimishwa nchini Panama kuanzia tarehe 22- 27 Januari 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema”. Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu, ameongoza Ibada ya Misa Takatifu Parokiani hapo majira ya jioni! Wakati wa Ibada ya Misa ya Asubuhi, Kardinali Angelo Comastri, Mwakilishi wa Baba Mtakatifu kwa mji wa Vatican, katika mahubiri yake alikazia umuhimu wa wazazi kutekeleza dhamana na wajibu wao wa m...