Balozi wa Papa awasili nchini

n Na Bernard James

BALOZI wa Vatikani nchini Tanzania Askofu Mkuu Marek Solczyński amewasili nchini Julai 12, majira ya sa 9 usiku, huku akilakiwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya.
Aidha Balozi huyo mpya amelakiwa na Katibu Mkuu wa Balozi wa Vatikani nchini Daniel Pacho, Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Askofu Alfred Maluma wa Jimbo Katoliki Njombe, Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padri Daniel Dulle, wawakilishi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam na baadhi ya watendaji wa TEC.
Kabla ya kuteuliwa kuja nchini, Askofu Mkuu Solczyński alikuwa Balozi wa Vatikani nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.



Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU