JIMBO LAZINDUA BIBLIA KATOLIKI ILIYOANDIKWA KATIKA LUGHA ZA ASILI



Jimbo Katoliki Solwezi nchini Zambia limezindua Biblia iliyotafsiriwa katika lugha tatu za asili nchini humo, Kaonde, Lunda na Luvale. Lugha hizo zinatumika zaidi katika Jimbo Katoliki Solwezi.
Akizungumza katika Homilia yake kwenye Parokia ya Mt. Daniel (Kanisa Kuu), Askofu wa Jimbo hilo Mhashamu Charles Kasonde amesema wakristo wanahitaji kuimarisha ufahamu wao wa neno la Mungu kwa kulifanya kuwa mtindo wao wa maisha ya kikristo.
Katika Misa takatifu iliyoendana na uzinduzi wa Biblia hiyo, Askofu Kasonde amekabidhi biblia kwa waamini 6, wa kike(3), waume 3. Pia amewakabidhi watoto wawili katika misa hiyo, ikiwa ni ishara ya Neno la Mungu kupita katika kizazi kimoja hadi kingine.

Bernard James

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU